Una mahusiano na mwanaume au mwanamke ambaye kimsingi mpo katika
uchumba. Unampa zawadi nyingi naye anakupa zawadi. Mnayo ahadi ya kufunga ndoa
na kuishi kama mme na mke . Na kwasababu hiyo unajitoa sana kimatumizi kwa mtu
huyo.
Lakini katika mazingira usiyoyaelewa unaona sasa mambo hayaendi vizuri.
Hayaendi vizuri katika kiwango ambacho sasa mahusiano yamevunjika kabisa.
Hakuna tena mahusiano. Au bado yapo lakini kwa mambo unayofanyiwa unaona kabisa
hutakiwi tena.
Kumbuka huko nyuma umegharamia sana. Umegharamia kwa fedha na mali.
Swali ni je vitu hivi haviwezi kurudishwa ?. Vitu hivi haviwezi kufidiwa ?. Na
je sheria imeongelea kuhusu jambo hili ?.
Majibu ya maswali haya yote ni ndiyo. Ni ndiyo, na gharama pamoja nazo
zawadi zinaweza kurejeshwa. Unaweza kushangaa kuona sheria imeongelea hata
mambo ya uchumba lakini ndio ukweli.
Wengi tunaijua sheria katika kuongelea wizi, dhamana, mikataba,
mirathi, ndoa, na mengine. Lakini ni vyema tukajua kuwa sheria ni pana na
imeongelea mambo mengi mno. Hili la uchumba nalo ni sehemu ya yaliyoongelewa.
No comments:
Post a Comment