SHIRIKISHO
la Sanaa za Maonesho Tanzania (SHISTAMA) linajipanga kupeleka mpango kazi wake
kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kabla ya uzinduzi wa Shirikisho hilo.
Akizungumza
na Wor’Out
Media jana, Rais wa Shistama, William Chitanda ‘MC Chitanda’ baada
ya mipangilio kutoka BASATA, watatengeneza Kalenda itakayokuwa na mgawanyo wa
majukumu ya Shirikisho hilo.
MC
Chitanda alisema mikakati mingine watakayoitekeleza ni kuwatambua na kuongeza
idadi ya wanachama wenye usajili unaotambulika na Shirikisho hilo.
“Tunatambua
baadhi ya wasanii wengine hawajajiunga katika vyama ili Shirikisho liwe na
nguvu ambayo itasongesha mbele maendeleo ya Shirikisho”, alisema MC Chitanda.
MC
Chitanda alisema mikakati yao itafanikisha kukuza na kuendeleza uchumi ambako
pia wanajipanga kuunda miradi kama SACCOS na Benki ya Wasanii.
No comments:
Post a Comment