Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati)
akizungumza na wananchi kwenye siku ya kilele cha Maadhimisho ya miaka 110 ya
vita vya Maji Maji na uzinduzi wa Makumbusho ya Hayati Rashidi Kawawa
yaliyofanyika mkoani Ruvuma katika wilaya ya Songea. Wengine ni Mkuu wa mkoa wa
Ruvuma, Dkt. Binilis Mahenge (wa pili kulia) Mbunge wa viti maalum wa Ruvuma,
Jacquiline ngonyani (wa kwanza kulia) Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon
Kochanke (wa kwanza kushoto) pamoja na Chifu wa wangoni, Emanuel Zulu (wa pili
kushoto).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akiwa na Mkuu wa
Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilis Mahenge wakiangalia baadhi ya Nishani alizokuwa
akitunukiwa Dkt. Rashid Mfaume Kawawa katika kulitumikia taifa kwa uzalendo
mara baada ya kuzinduzia jana Makumbusho ya Hayati Rashidi Kawawa yaliyofanyika
mkoani Ruvuma katika wilaya ya Songea.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto)
akizungumza na mtoto wa wa Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa, Vita Kawawa (wa
kwanza kushoto) mara baada ya kuangalia baadhi ya vitabu vya Hayati Kawawa
alivyokuwa akivipenda kuvisoma enzi za uhai wake vilivyopo katika Makumbusho ya
Hayati Rashidi Kawawa baada ya kuzindua makumbusho hayo iliyofanyika jana
mkoani Ruvuma katika wilaya ya Songea.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akiweka silaha ya
jadi (rungu) kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa waliouawa kwa kunyongwa na
wakoloni kwenye siku ya kilele cha Maadhimisho ya miaka 110 ya vita vya Maji
Majiyaliyofanyika mkoani Ruvuma katika wilaya ya Songea Balozi wa Ujerumani
nchini Tanzania
Mbunge wa viti maalum wa Ruvuma (CCM) Jacquline Ngonyani akiweka silaha
ya jadi (rungu) kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa waliouawa kwa kunyongwa
na wakoloni kwenye siku ya kilele cha Maadhimisho ya miaka 110 ya vita vya Maji
Majiyaliyofanyika mkoani Ruvuma katika wilaya ya Songea Balozi wa Ujerumani
nchini Tanzania
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof.Jumanne Maghembe (wa tatu kulia)
akiwa na Chifu wa Kabila la wangoni, Emmanuel Zulu (wa pili kulia) wakiwa
kwenye maandamano ya siku ya kilele cha Maadhimisho ya miaka 110 ya vita vya
Maji Maji na uzinduzi wa Makumbusho ya Hayati Rashidi Kawawa yaliyofanyika
mkoani Ruvuma katika wilaya ya Songea. Wengine ni Mwenyekiti wa Machifu wa
nchini, Chifu Fundikila (kulia) pamoja na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania,
Egon Kochanke (wa pili kushoto).
No comments:
Post a Comment