Hakuna ambacho
kinaongeza joto katika mwili wa binadamu wakati wa baridi kama chai ya
tangawizi.
Kutokana na kiwango
chake cha juu cha Vitamin C, magnesiamu na madini mengine, tangawizi ni ya
manufaa sana kwa afya ya bianadamu.
Tangawizi ni mmea
ambao hutumika kama kiungo na pia hujulikana kwa sifa yake ya kutumika kama
tiba.
Inaweza kutumika
kama unga,kama mafuta, juisi au chai.
Tangawizi
inafahamika sana kwa sifa yake ya ajabu ya kutibu magonjwa.
Tangawizi ni nzuri
kutumiwa kama chai, tangawizi ni chanzo kizuri cha vitamini na madini kama vile
vitamini C na magnesiam.
Kuna faida nyingi
utakazozipata kwa kunywa chai ya tangawizi:
1. Huzuia Magonjwa ya
Mtingishiko
Chai ya
Tangawiziinawezakuzuiakutapika na kumaliza maumivu ya kichwa. Pia inazuia
kichefuchefu kinachotokana na mitingishiko ya safari za gari, meli au ndege. Hivyo
kunywa kikombe kimoja cha tangawizi kitaweza kusaidia kuepuka kichefuchefu na
kutapika.
2. Inazuia Mchafuko wa Tumbo
Chai ya Tangawizi
inasaidia mmengenyo wa chakula tumboni hivyo kuongeza kunyonywa kwa chakula
tumboni na kuzuia maumivu ya tumbo yanayotokana na kula chakula kingi.
Pia huongeza hamu
ya kula.
3. Hupunguza
Uvimbe
Tangawizi chai
inaweza kupunguza uvimbe wa viungo unaojulikana kama rheumatoid arthritis.
4. Hupambana
na Magonjwa ya Kupumua.
Unashauriwa kunywa
tangawizi kama unasumbuliwa na magonjwa ya kupumua kama vile mafua na kikohozi.
5. Huchochea
Mzunguko wa Damu
Kunywa kikombe cha
chai ya tangawizi kunaweza kukusaidia kuboresha mtiririko wa damu, kama vile
kusaidia kuzuia mafua na homa.
6. Huongeza
Kinga za Mwili
Chai ya Tangawizi
ina chemikali za antioxidants zinazosaidia kuboresha mfumo wa kinga.
Kunywa kikombe cha
chai ya tangawizi kila siku kunaweza pia kusaidia kuondokana na hatari ya
kiharusi kwa kuzuia mafuta katika kuta za mishipa ya damu. Tangawizi pia
imeonyesha mafanikio katika kupunguza viwango vya rehani (Chorestrol) na kuzuia
kansa.
7. Hutuliza
Msongo wa Mawazo
Tangawizi ina uwezo
mkubwa wa kupunguza msongo wa mawazo kwa harufu yake nzuri ya kuvutia.
8. Inapunguza
Matatizo ya Tumbo:
Inachochea kasi ya
mmengenyo wa chakula kwa kuchangia kutolewa kwa asidi katika tumbo. Tangawizi
inaweza kutumika kushughulikia tatizo la kukosa choo.
9. Husaidia
Katika Kupunguza Maumivu:
Tangawizi chai
inaweza kupunguza maumivu ya mwili na misuli.
Kunywa kikombe
chachai ya tangawizi kila siku kunaweza kusaidia kuzuia maumivu yamisuli pia
kusaidia kupunguza uchovu wa mwili.
10. Husaidia
kwa Kuondoa Ugonjwa wa Asubuhi
Husaidia kupungua
kichefuchefu kwa akinamama wajawazito kunakotokakna na ugonjwa wa asubuhi kwa
kizungu “Morning Sickness”
11. Huboresha
Nguvu za Uzazi kwa Wanaume
Tangawizi inasaidia
kuboresha mbegu za kiume na nguvu za uzazi kwa wanaume kama ikitumiwa mara kwa
mara. Pia inasaidia kutibu upungufu wa nguvu za kiume.
12. Kupunguza
Uzito wa Mwili:
Tangawizi inasaidia
sana katika kupunguza uzito wa mwili. Inasaidia kuunguza mafuta ya ziada katika
mwili.
13. Kuongeza
hamu ya Kula
Tangawizi inasaidia
kuongeza hamu ya kula kwa kuchochea kutengenezwa kwa asidi za kumengenya
chakula katika tumbo.
14. Husaidia kutoa Gesi.
Tangawizi inasaidia
kutoa gesi chafu tumboni kwa njia ya asili.
15. Inasaidia
Kupumua Vizuri.
Tangawizi inasaidia
kufungua njia ya hewa na kukufanya upumue vizuri. Unaweza kuitumia baada ya
kula kama kiburudisho pia.
Wanawake wajawazito
na wale wenye tatizo la kutokwa na damu kirahisi wanashauriwa kupata ushauri wa
Daktari kwanza kabla ya kutumia chai ya Tangawi
No comments:
Post a Comment