Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Dkt. John Jingu (kulia) akizungumza na
wdau kutoka Shirika la PCI alipokutana nao kujadiliana masuala mbalimbali
yakiwemo kumuwezesha mwanamke kiuchumi, usawa wa kijinsia na maendeleo ya mtoto
ofisini kwake jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya
Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike (kulia) akieleza jinsi Idara ya
Maendeleo ya Jamii kupitia Maafisa Maendeleo ya Jamii wanavyoweza kushirikiana
na wadau mikoani kumuwezesha Mwanamke kiuchumi wakati wa kikao
kilichowakutanisha wadau hao na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto ( Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Dkt. John Jingu ofisini
kwake jijini Dodoma.
Mshauri wa Masuala ya Kitaalam kutoka Shirika la PCI Bi.
Lindsay Harnish (kulia) akieleza kuhusu Elimu zinazotolewa na Shirika hilo nje
ya Mradi wa kumuwezesha Mwanamke Kiuchumi wakati wa kikao kilichowakutanisha
wadau hao na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto ( Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Dkt. John Jingu ofisini kwake jijini
Dodoma.
Meneja Mradi wa Kumuinua Mwanamke Kiuchumi kutoka Shirika la
PCI Bw. Hillary Dashina (wa tatu kulia)akielezea kuhusu mradi wa kumuwezesha
Mwanamke Kiuchumi katika mikoa ya Mara na Arusha ambapo mpaka sasa umewezesha
zaidi ya wanawake 10,000 katika mikoa hiyo wakati wa kikao kilichowakutanisha
wadau hao na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto ( Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Dkt. John Jingu ofisini kwake jiijini
Dodoma.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Mkoa wa Mara Bi. Neema Ibamba
(katikati) akielezea jinsia Shirika la PCI limesaidia sana jamii ya Mkoa wa
Mara hasa Wakurya kubadili fikra zao juu ya Mwanamke na Mtoto wa kike katika
kikao kilichowakutanisha wadau hao na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya
jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Dkt. John Jingu
ofisini kwake jiijini Dodoma.
Jumla ya Wanawake 12,309 kutoka mikoa ya Mara na Arusha wamenufaika na Mradi wa kumuwezesha Mwanamke Kiuchumi unaotekelezwa katika mikoa hiyo na Shirika la PCI kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi za mikoa husika.
Hayo yamebainika katika kikao kilichowakutanisha Wadau kutoka Shirika la PCI na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Dkt. John Jingu alipokutana na wadau hao kujadiliana masuala mbalimbali yakiwemo kumuwezesha mwanamke kiuchumi, usawa wa kijinsia na maendeleo ya mtoto.
Akizungumza katika kikao hicho Meneja Mradi wa kumuwezesha Mwanamke Kiuchumi kutoka Shirika la PCI Bw. Hillary Dashina amesema kuwa Mradi huo umeanzishwa kwa lengo la kumuwezesha mwanamke kiuchumi hasa mwanamke aliyeishi kijijini.
Ameongeza kuwa mpaka sasa Mardi huo unatekelezwa katika Mikoa miwili ambayo ni Arusha na Mara na katika mikoa hiyo Mradi huo unatekelezwa katika Wilaya za Longido na Monduli kwa Mkoa wa Arusha na Wilaya za Butiama, Bunda na Musoma kwa mkoa wa Mara.
Ameeleza kuwa mradi huo kwa mkoa wa Arusha una jumla ya vikundi 151 katika mkoa huo ikiwa vikundi 77 katika wilaya ya Longido na vikundi 74 katika wilaya ya Monduli na vikundi 445 katika mkoa wa Mara ikiwa vikundi 140 katika Wilaya ya Bunda vikundi 164 katika Wilaya ya Musoma na vikundi 141 katika Wilaya ya Butiama.
“Katika mradi huu tunamuzesha Mwanamke zaidi ya kumuwezesha kichumi pia tunatoa mafunzo ya kuanzisha na kuendeleza biashara kitaalamu na zaidi ya wanawake 500 wamepatiwa mafunzo hayo” alisema
Bw. Dashinda ameongeza kuwa katika kutekeleza mradi huo pia wametoa elimu ya stadi za maisha kwa zaidi ya wanawake 7000 ambayo imewawezesha kujikwamua kiuchumi na kutatua changamoto mbalimbali katika familia na jamii zao.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Dkt. John Jingu amesema Serikali ipo tayari kuendelea kushirikana na Shirika hilo katika kuhakikisha Mwanamke anakombolewa hasa katika Nyanja ya kiuchumi ili kuwezesha kuwa na taifa lenye maendeleo kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
Ameongeza kuwa ni muhumu kwa Shirika hilo na Mashirika mengine yanayofanya kazi ya kumuwezesha Mwanamke kiuchumi kuwekea mkazo katika matumizi ya teknolojia katika kuhakikisha wanawake wanapata elimu na fursa mbalimbali za kijikwamua kiuchumi.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Mkoa wa Mara Bi. Neema Ibamba amesema kuwa Shirika la PCI limesaidia sana jamii ya Mkoa huo hasa Wakurya kubadili fikra zao juu ya Mwanamke na Mtoto wa kike na kwa sasa wanaume wamekuwa wakishiriki katika masuala ya kumuwezesha Mwanamke na mtoto wa kike.
No comments:
Post a Comment