Ofisa wa Bima wa Benki ya NBC, Catherine Ngowi (kulia) akitoa elimu ya masuala ya bima n aina mbalimbali ya huduma za bima zitolewazo na NBC kwa ammoja wa wateja wa benki hiyo, Miryam Mjema ikiwa ni moja ya matukio katika kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo mjini Dar es Salaam hivi karibuni. Wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Bima wa benki hiyo, Benjamin Nkaka na ofisa mwingine wa NBC, Batuli Kassim.
Ofisa wa Bima wa benki ya NBC, Emarynziana Mtega (kulia), akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kujiwekea bima na aina mbalimbali ya huduma za bima zitolewazo na NBC kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo kutoka Kampuni ya Mogas Tanzania Ltd, Grayson Kazeni kiwa ni moja ya matukio katika kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo mjini Dar es Salaam hivi karibuni.
Maofisa wa benki ya NBC, wakizungumza na wateja wakati wakitoa elimu kuhusu masuala ya bima kwa wateja ikiwa ni moja ya matukio ya maadhimisho ya Mwezi wa Huduma kwa Wateja jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakipozi kwa picha ya kumbukumbu katika hafla hiyo. Wafanyakazi hao walitoa elimu ya bima ikiwa ni pamoja na bidhaa mbalimbali za bima zitolewazo na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja wa NBC.
NA Mwandishi wetu;
BENKI ya NBC imeendelea kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja kwa kufanya matukio sehemu mbalimbali nchini na hapo jijini Dar es Salaam ikitoa elimu kuhusu umuhimu wa bima na pia ikiwaleleza wateja aina mbalimbali ya huduma za bima zitolewazo na benki hiyo.
Akizungumza katika tukio hilo, Mkuu wa Kitengo cha Bima wa NBC, Benjamin Nkaka alisema watanzania wanapaswa kuwa utamaduni wa kujiwekea bima wao pamoja na watoto wao dhidi ya matukio na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza wakati wowote.
Akitoa mfano wa bima hizo ni bima ya elimu ya Educare itolewayo na inayomuwezesha mzazi kuweka akiba kidogokidogo kwa ajili ya elimu ya mtoto wake pindi yatokeapo majanga yanayoweza kusababisha ulemavu wa kudumu ama kifo.
“Tumekwishakuwa na huduma hii, tunachotaka sasa ni kwa wateja kuweza kuielewa vivuri, na ndio maana tumendaa hafla kama hii ili kuwafahamisha wateja wetu na wananchi kwa ujumla huduma ya bima ya elimu ya NBC inavyoweza kumkomboa mteja,” alisema.
Alisema kwa kupitia huduma hii mteja humwekea akiba mtoto wake kidogokidogo kwa kiasi atakachopanga kwa mkataba wa muda kuanzia miaka saba hadi 18 ili kugharamia elimu ya mtoto wake.
“Bima hii ya elimu ni mpango ambao mzazi huweka akiba kila mwezi
hivyo kuleta faraja moyoni kwamba endapo chochote kitatokea iwe ulemavu wa
kudumu ama kifo kabla ya muda huo basi bima itagharamia elimu ya mtoto wako.
“Kiwango cha chini ni miaka saba hadi 18 na kiwango cha chini
cha kuwekeza katika mpango huu kwa mwezi ni shs 7,500/- hakuna kiwango
cha mwisho cha juu. Uwekezeji katika elimu ya mtoto ni jambo pekee katika
kuhakikisha malengo ya kielimu ya mtoto yanatimia ,” aliongeza Bwana Nkaka.
No comments:
Post a Comment