Dar es Salaam: Promosheni ya Paka Rangi ya Plascon
na Ushinde imerejea, na sasa inakuja na toleo maalumu la rangi, maarufu kama
Rangi ya Pesa kwa nia njema ili kuwanifaisha wateja wake. Mwaka huu washindi
watajishindia na zawadi za pesa taslimu.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo,
Hussein Jamal, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo kipya
cha mauzo ya rangi ya Plascon, jijini Dar es Salaam. Jamal alisema, “Kibiashara
tunafurahi kuwa na kampeni kama hii ambapo kupitia katika promosheni yetu ,
tuna uhakika kwamba, kuwapo na ushindi wa pesa taslimu kutaleta nyuso za furaha
kwa washindi katika kipindi chote cha msimu wa kampeni hii.
Promosheni ya Paka Rangi na Ushinde inatupatia fursa, siyo tu
kuwazadia wateja wetu muhimu, watumiaji wa rangi na wauzaji, lakini pia kujenga
msingi wa mafanikio ambayo tumeyapata kupitia bidhaa yetu ya hii ya Plascon,
tangu tulipoizindua mwaka 2017,”
Kadhalika, Jamal alifafanua kuwa, promosheni hiyo ni ushahidi
tosha wa kuonesha jinsi ambavyo Plascon imeamua kutoa huduma kwa watanzania na
namna biashara yake inavyolenga kuongeza thamani katika uzalishaji wa rangi
bora, zenye viwango, utafiti na wenye lengo la kukidhi haja ya mahitaji ya
rangi na kutoa ushauri bora kwa watanzania na watumiaji wa rangi kwa ujumla.
Promosheni iliyopewa jina la ‘Colour of Money’ itaendeshwa
kuanzia Otoba 7 hadi Desemba 14, 2019, na inatarajia kushirikisha mamia na
maelfu huku kila mshiriki akiwa na uhakika wa kutotoka mikono mitupu. Meneja
Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Tyron Immelmann, alisema kuwa, mwaka huu,
Plascon itatoa zawadi za pesa taslimu shilingi milioni tano kila wiki, ambapo
kila siku kutakuwa na mshindi wa Sh 1,000,000 taslimu.
Washiriki watatakiwa kununua lita 20 za rangi ya Plascon, na
kupewa kadi ambayo mteja ataisugua na na kutuma namba zake za bahati kwenda
15054, baada ya hapo atakuwa katika nafasi nzuri ya kuibuka mshindi. Matangazo
ya Msimu huu wa Promosheni ya Paka Rangi Ushinde na Rangi ya Pesa, yatatangazwa
kupitia vipeperushi kutoka kwa wauzaji, halikadhalika kupitia katika radio na
televisheni.
No comments:
Post a Comment