RC MAKONDA AWAPA SIKU TANO WAKANDARASI "WABABAISHAJI" KUHAKIKISHA WANATEKELEZA MIRADI YAO, AWAONYA WATAKAOKAIDI AGIZO - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, October 22, 2019

RC MAKONDA AWAPA SIKU TANO WAKANDARASI "WABABAISHAJI" KUHAKIKISHA WANATEKELEZA MIRADI YAO, AWAONYA WATAKAOKAIDI AGIZO


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewapa Siku tano kuanzia leo October 22 Wakandarasi ambao miradi yao imekuwa ikisuasua kuhakikisha wanaanza kazi mara moja na kubainisha kuwa wakandarasi watakaokaidi agizo hilo Watakamatwa na Vyombo vya dola na Mikataba yao kuvunjwa.

RC Makonda amesema wapo wakandarasi ambao Walidanganya kwenye nyaraka za kuomba tenda kuwa wana Vifaa vya Kutosha, Wataalamu na Fedha za kutosha ili waatiwe kazi lakini baada ya kupata kazi wamekuwa wakikwama kufanya kazi kutokana na uhaba wa Vifaa jambo linalopelekea miradi kutokamilika kwa wakati na kuleta Usumbufu kwa wananchi.

Aidha RC Makonda amezionya Bodi za Manunuzi zitakazobainika kutoa tenda kwa wakandarasi kwa rushwa bila kuangalia uwezo wa Kampuni kuwa watachukuliwa hatua.

Miongoni mwa Miradi ambayo RC Makonda amesema imekuwa ikisuasua ni Ujenzi wa Mto Ng'ombe, Mfereji wa Buguruni Kisiwani, Tabata Roman Catholic,  Barabara ya Kivule na Barabara ya Kawe.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages