Madiwani Namtumbo Walalamikia Korosho Zao Kuuzwa Tunduru - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, April 2, 2021

Madiwani Namtumbo Walalamikia Korosho Zao Kuuzwa Tunduru

Diwani wa kata ya magazini Grace Kapinga akiwasilisha malalamiko ya kuuzia zao la korosho wilaya ya Tunduru na kutaka zao hilo liuziwe chama kikuu cha SONAMCU na sio TAMCU.

Na Yeremias Ngerangera, Namtumbo | Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wamelalamikia kitendo cha wakulima wa korosho wilayani Namtumbo kupeleka korosho zao wilaya ya Tunduru katika chama kikuu cha TAMCU kila mwaka badala ya kuuzia Namtumbo katika chama kikuu cha SONAMCU.

Wakiongea katika kikao cha kamati ya fedha uongozi na mipango cha Halmashauri hiyo diwani wa kata ya Magazini Grace kapinga alidai kitendo cha wakulima wetu, sisi wenyewe kuendelea kuuza mazao katika chama kikuu cha wilaya ya Tunduru TAMCU sio sahihi.

Grace alisema kiwango kinachozalishwa korosho katika wilaya ya Namtumbo ni kikubwa sana hakuna sababu ya kuendelea kupeleka korosho hizo katika wilaya ya Tunduru kwa kuwa kuna chama kikuu SONAMCU wanaweza kununua korosho hizo katika wilaya yetu kama wanavyofanya mazao ya stakabadhi ghalani alisema kapinga.

Afisa kilimo na ushirika wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Joseph Mbilinyi alidai uwezekano wa kuuzia katika chama kikuu cha SONAMCU utakuwepo endapo uzalishaji wa zao la korosho katika wilaya ya Namtumbo utavuka tani 1000 na kuwepo kwa maghala ya kuhifadhia korosho wakati wa mauzo.

Bwana Mbilinyi pamoja na mambo mengine alisema hana tatizo na kuwepo kwa maghala ya kuuzia zao la korosho katika wilaya ya Namtumbo bali tatizo ni kukidhi kigezo cha kuwa na uzalishaji unaoanzia tani 1000 na kuendelea kadiri ya mwongozo.

Afisa ushirika wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Emmanuel Gwao alitoa takwimu za uzalishaji wa zao la korosho za kutoka wilaya ya Namtumbo zilizouzwa wilaya ya Tunduru kwa msimu wa 2020/2021 kuwa ni tani 321 na kg 931 na tani 500 kwa musimu wa 2019/2020.

Hata hivyo aliongeza kuwa wapo wananchi katika vijiji vya wilaya ya Namtumbo wanaozalisha korosho kwa kiwango kidogo hawapeleki katika masoko kutokana na umbali wa kuuzia zao lenyewe hivyo kama kutakuwa na utaratibu wa kupata soko la kuuzia korosho wilayani Namtumbo tutawashawishi wananchi wengine wasio katika mfumo rasmi wa kuuza zao la korosho kujiunga katika mfumo rasmi ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kukidhi vigezo vya kufika kilo 1000 zinazohitajika.

Naye diwani wa kata ya Limamu Isdory Nyati alisisitiza swala la ukusanyaji wa mapato hasa kwa kuhakikisha mabasi yanayotumika kubeba mazao kudhibitiwa huku akiyataja mabasi hayo kuwa ni Kangaulaya na Kisumapai yanayofanya biashara ya kubeba abiria na mizigo kutoka mamlaka ya mji mdogo wa Lusewa kwenda Songea na kuipotezea ushuru Halmashauriya wilaya ya Namtumbo.

Katibu tawala wa wilaya ya Namtumbo bwana Aden Nchimbi pamoja na kuwapongeza madiwani hao kwa kufuatilia kwa makini magari ya abiria yanayotumika kubeba mizigo badala ya kubeba abiria kuwa atahakikisha anasimamia swala hilo kwa makini ili kudhibiti magari hayo yasiendelee kufanya hivyo.

Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ina tegemea ushuru wa mazao katika ukusanyaji wake wa mapato na kuwepo kwa mianya ya utoroshaji wa mazao kwa njia ya mabasi inaipotezea ushuru Halmashauri wilaya ya Namtumbo na kupeleka songea.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages