Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deogratius Ndejembi (kushoto) akiangalia Kadi maalum ya malipo (Prepaid Eazy Card) ya Benki ya Equity alipofanya ziara ya kutembelea Banda la Benki hiyo kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam. (katikati) ni Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Benki ya Equity Godwin Semunyo na (wa kwanza kulia) ni Meneja Huduma kwa Wateja wa Benki hiyo Sarah Mujule.
Meneja Huduma kwa Wateja wa Benki ya Equity Sarah Mujule (kulia) akimkabidhi Kadi maalum ya (Prepaid Eazy Card) ya Benki hiyo Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deogratius Ndejemb (kushoto) alipofika kwenye Banda la Benki hiyo kujionea huduma mbalimbali zitolewazo na Benki hiyo kwenye maonesho ya Sabasaba.
Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Benki ya Equity Bw. Godwin Semunyo (wa pili kulia) akitoa maelezo kuhusu Kadi hiyo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deogratius Ndejembi (katikati) aliyefanya ziara kwenye Banda lao. (wa kwanza kushoto) ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki Benki ya Equity Geofrey Magugi, na (wa kwanza kulia) ni Meneja Huduma kwa Wateja wa Benki hiyo Sarah Mujule.
Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Benki ya Equity Bw. Godwin Semunyo akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) juu ya Kadi mpya ya malipo ya Benki hiyo (repaid Eazy Card) namna inavyofanyakazi na kuweza kuwasaidia wananchi wengi kwa kuweka akiba na kufanya manunuzi popote bila ya kuwa na Account kwenye Benki hiyo.
Meneja Mahusiano Kitengo cha Biashara Benki ya Equity David Mnkande (wa kwanza kushoto anaendika) akiwa na Meneja Mtendaji wa Benki hiyo Anastella Mchomba (kushoto kwake) wakimhudumia mteja aliyefika kwenye Banda lao kupata huduma mbalimbali kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mahusiano Uwakala wa Benki ya Equity (mwenye laptop) akimsikiliza Mteja aliyefika kwenye meza yake kupata huduma ndani ya Banda la Benki hiyo kwenye Maonesho ya Sabasaba. (PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)
Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM | Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deogratius Ndejembi ametembelea Banda la Benki ya Equity katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere na kuipongeza Benki hiyo kuja na Kadi ya Prepaid Eazy Card ambayo inaweza kusaidia kupunguza matumizi ya fedha lakini pia kusaidia watu wengi kuweza kumiliki kadi hasa kwa kufanya miamala kwenye mitandao ambayo imekuwa ni changamoto kwa watu wanaofanya miamala mitandaoni.
Amesema kuwa Benki hiyo imebadili mtazamo wake kuwa Benki ya wananchi hasa kuiwezesha jamii kuweza kumiliki Kadi hiyo kwa kujiwekea akiba kwenye Kadi hiyo na kuweza kufanya manunuzi popote alipo.
“Jambo hili lililofanywa na Benki ya Equity ni jambo zuri hii itawawezesha wananchi wengi kuweza kumiliki Kadi hii na kuweza kujiwekea akiba na kufanya matumizi popote anapokuwepo lakini vilevile litasaidia kuweza kutunza matumizi ya fedha na kuwasaidia wengi kuingiakatika hatua ya kumiliki Kadin a kufanya miamala ya kwenye mitandao.” Amesema Mhe.Ndejembi.
Aidha ameiopongeza Benki hiyo kwa kuweza kutoa mikopo kwa makundi mbalimbali ya wanawake na vijana kwa kuunda vikundi na kuweza kupatiwa mikopo kutoka Benki hiyo ambapo mpaka sasa vijana wengi wamenufaika na mikopo yao na kwamba kwa kufanya hivyo wameweza kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwawezesha vijana hao ambao ni nguvukazi ya Taifa.
“Serikali tayari tunatoa ile mikopo ya vikundi asilimia 10 inayotengwa na halmashauri kwa maana asilimia 2 ya walemavu, asilimia 4 ya wakina mama na asilimia 4 ya vijana lakini kwa kushirikiana na Taasisi za kifedha kama hii Equity naamini kwamba sasa ule mwarobani kwamba vijana wengi kulalamika kutokuwa na mitaji unaenda kuisha kwasababu mitaji sasa ipo ni wao sasa kujitambua na kujielewa”. Amesema Mhe.Ndejembi.
Nae Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Benki ya Equity Bw.Godwin Semunyo amewakaribisha wananchi kwa ujumla kutembelea banda lao kuweza kupata huduma za kifedha kupitia Benki hiyo ambayo ni Benki ya wananchi.
Aidha Bw.Semunyo amesema kuwa uwepo wa Kadi ya Eazy Card ambayo inapatikana kwa bei ya shilingi elfu 10 ambapo mteja ataingizia fedha kwa njia tofauti na kuweza kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao au mawakala wao.
“Kadi ya Ezy-Card ni kadi ambayo unaweza ukaitumia kwenye ATM zote zinazopokea nembo za visa hapa Tanzania, tunazungumza zaidi ya ATM 3,000 lakini pia kwenye maneo ya kupokea malipo ya kadi kwahiyo ni kadi ambayo unaweza ukaitumia kwa urahisi na popote Tanzania”. Amesema Semunyo.
No comments:
Post a Comment