JATU PLC YAWAOMBA WANANCHI DAR KUTEMBELEA BANDA LAO LILILOPO MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, July 1, 2021

JATU PLC YAWAOMBA WANANCHI DAR KUTEMBELEA BANDA LAO LILILOPO MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA

Wananchi wakiwa katika banda la JATU PLC wakipata maelezo kabla ya kununua hisa za kampuni hiyo.JATU wapo katika maonesho ya 45 ya biashara ya kimaifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu Sabasaba wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam.
Maofisa wa Kampuni ya JATU PLC wakimhudumia mmoja ya wananchi aliyefika kwenye banda lao kwa ajili ya kununua hisa za kampuni hiyo.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam | KAMPUNI ya JATU PLC imewaomba wananchi wanaotembelea Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa kutembelea banda la kampuni hiyo ili kupata taarifa mbalimbali zinazohusu namna ya wananchi kujikomboa kiuchumi kupitia kauli mbiu inayosema Buku Tano inatosha.

Akizungumza na Michuzi Blog na Michuzi TV Ofisa Masoko wa Kampuni ya JATU PLC Ngorosho Winfrida amesema huu ni wakati muafaka wananchi wanaokwenda kutembelea maonesho hayo wakafika banda la JATU na wakiwa hapo watapewa maelezo ya umuhimu wa kununua hisa ili kubadilisha maisha yao kiuchumi.

Amefafanua kwamba JATU PLC wapo kwenye viwanja vya Sabasaba yanakoendelea maonesho hayo na kazi wanayoendea nayo ni kuhamasisha wananchi kununua hisa na kauli yao ni Buku tano inatosha na kiasi hicho cha fedha kinatosha kumfanya mwananchi kununua hisa.

Ameongeza "Tunaomba wananchi wafike kwenye banda la JATU PLC, tuko kwa ajili yao na kwa wale ambao watanunua hiisa zetu watapata fursa ya kujikomboa kiuchumi kwani baada ya kununua hisa tutawapa fursa za kushiriki kikamilifu katika shughuli za kujikomboa kiuchumi kupitia kilimo na shughuli nyingine zitokanazo na kilimo pamoja na nafaka."

"JATU tupo kwenye viwanja hivi vya Mwalimu Nyerere Sabasaba na kubwa zaidi tumekuja na kauli mbiu yetu ya Buku tano inatosha ambapo fedha hiyo itamwezesha mwananchi kununua Hisa."

Aidha Ngorosho amesema kampuni hiyo ni Mtanzania na lengo lake kubwa ni kushirikiana na jamii ya Watanzania kupata fursa ya kushiriki katika shughuliza kiuchumi na hatimaye kujikomboa kiuchumi,na kubwa zaidi amedhamiria kufanya mageuzi katika sekta ya kilimo.

Pia Ngorosho amesema kwa sasa wapo hatua za mwisho kwani kampeni yao inayosema Buku Tano inatosha inatarajia kumalizika mwishoni mwa Julai, 2021, hivyo ni vema wakachangamkia kununua hisa za kampuni hiyo hasa katika siku zilizobakia.

"JATU PLC licha ya mambo ya hisa lakini imejikita kwenye kilimo ambapo tunajihusisha na shughuli za kilimo katika maeneo karibu yote nchini Tanzania, lakini tunayo masoko kwa ajili ya bidhaa za nafaka ambayo yapo ndani na nje ya Tanzania, hivyo tunayo masoko ya uhakika a ukiwa na hisa za kampuni yetu mwana hisa anayo nafasi ya kuchagua anataka kujikita kwenye eneo gani," amesema Ngorosho.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages