Naibu Waziri Sagini Afanya Ziara Mkoani Mara, Akutana Na Mkuu Wa Mkoa Na Kamati Ya Ulinzi Na Usalama - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, January 22, 2022

Naibu Waziri Sagini Afanya Ziara Mkoani Mara, Akutana Na Mkuu Wa Mkoa Na Kamati Ya Ulinzi Na Usalama

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. AllySalum Hapi akimuonyesha Naibu Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, Jumannne Saginiukarabati wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara iliyopo Manispaa ya Musoma, leo Mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani yaNchi, Jumanne Sagini akizungumza na Mkuuwa Mkoa wa Mara, Mhe. Ally Salum Hapikatika moja ya ziara zake katika ofisi ya Mkuuwa Mkoa huyo iliyopo Manispaa ya Musoma, mkoani Mara leo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani yaNchi, Jumanne Sagini akizungumza na Mkuuwa Mkoa wa Mara, Mhe. Ally Salum Hapikatika moja ya ziara zake katika ofisi ya Mkuuwa Mkoa huyo iliyopo Manispaa ya Musoma, mkoani Mara leo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani yaNchi, Jumanne Sagini amekutana naMwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoawa Mara, Samwel Kuboye, pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu CCM, Marakatika ziara yake Mkoani hapo leo,amewaomba washirikiane ili kudhibiti uhalifuuliopo mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani yaNchi, Jumanne Sagini akizungumza naWakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilayaya Butiama pamoja na Kamati ya Ulinzi naUsalama ya Wilaya ya Butiama leo, katikamoja ya ziara yake Mkoani Mara.
Na Mwandishi wetu, Mara | Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya NchiJumanne A. Sagini amefanya ziara mkoani Mara kwa kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi zaChama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara pamoja nakukutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama jimbonikwake Butiama.

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Ali Salum Hapi na Kamati ya Ulinzi naUsalama ya Mkoa huo, Sagini amesema kuwakwa nafasi yake ya Naibu Waziri wa Mambo yaNdani ya Nchi, jukumu lake kubwa ni kuhakikishausalama na amani ya nchi. Ameitaka Kamati yaUlinzi na Usalama kuendelea kushirikianakudhibiti uhalifu unaojitokeza.

Naibu Waziri Sagini aliyasema hayo jana, 21 Januari 2022 alipotembelea Ofisi ya Mkuu waMkoa wa Mara, Wilaya ya Musoma, mkoani Mara katika moja ya ziara yake.

Moja ya changamoto ninayolenga kuidhibiti nimatukio ya uhalifu yanayojitokeza mara kwa maraMkoani Mara na nchini kwa ujumla, hivyo navitakavyombo vya usalama kuongeza nguvu zaidikutokomeza matukio hayo."

Aidha Naibu Waziri Sagini ameshangazwa nakauli za baadhi ya wananchi wanaosema uhalifuutarudi kwa kasi kwasababu ya mawaziri wapyawa Mambo ya Ndani ya Nchi. Anasema IGP hajabadilishwa, Makamanda wa Polisi Nchi nzimani wale wale, sasa uhalifu utaongezeka kivipi?

Kuna maneno yanayosemwa kwamba uhalifuutarudi kwa kasi sasa hivi, naomba niwatoe hofukwani IGP ni yule Yule, Makamanda wa Polisi niwale wale, amani na usalama wa nchi utazidikuimarika

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mh, Ally SalumHapi amefurahia kwa ujio wake na kuahidi kutoaushirikiano unaohitajika katika kila sekta navyombo vya usalama vilivyomo katika Wizara yaMambo ya Ndani ya Nchi kwenye Mkoa wake.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages