
Ofisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini wakimsikiliza mkandarasi wakati walopokuwa wakikagua maendeleo ya ujenzi wa maskuli katika ziara yao hapo jana.

Moja ya jengo lililokaguiwa na watendaji wa Taasisi ya Ofisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini.

Taasisi ya Afisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (Presidential Delivery Bureau (PDB), kwa kushirikiana na Viongozi na Maafisa mbalimbali wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar wamefanya ziara ya kukagua Miradi ya Ujenzi wa Skuli za Serikali inayoendelea. Lengo la ziara hiyo ni kuangalia maendeleo ya Miradi hiyo.
Aidha wamewasisitiza Wakandarasi wa Majengo hayo kuhakikisha yanapatikana kwa wakati na kwa kiwango bora.
Katika ziara hiyo wametembelea ujenzi wa Skuli ya Chukwani, Maungani, Muungano, na Chumbuni - Unguja.
No comments:
Post a Comment