Kulia
ni Mwenyekiti wa mashindano ya Ritta Kabati challenge cup 2018 na
kushoto ni katibu wa kamati ya mshindano hayo walipokuwa wakiongea na
vyombo vya habari kwenye ofisi zao zilizopo manispaa ya Iringa mkoani
Iringa mapema hii leo
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Kamati ya ya mshindano ya Ritta
Kabati challenge cup 2018 imezindua rasmi kwa kuanza kuzialika timu kwa ajiri
ya kuchukua fomu kushiriki na wameweka bayana jinsi mfumo wa mashindano
utakavyokuwa pamoja na zawadi kwa washindi wote.
Akizungumza na waandishi wa
habari mwenyekiti wa mashindano hayo Gerald Malekela alisema kuwa analialika
timu mbalimbali za mkoa wa Iringa kuja kuchukua fomu za mashindano kwa gharama
ya shilingi elfu thelathini (30,000/=) ambazo zinapatikana katika kituo cha
radio cha Nuru Fm.
“Naomba viongozi wa vilabu
vinavyotaka kushiriki mashindano haya vinatakuwa kufika katika ofisi za Nuru fm
au kumpigia mratibu wa mashindano haya Fredy Mgunda kwa kumpigia simu ya
nambari 0714201006 au mnipigie mimi
mwenyewe kwa namba hii 0762687732 hapo utakuwa umerahisisha jinsi ya kuzipata
hizo fomu na maelezo kwa kina” alisema Malekela
Malekela alisema kuwa lengo la mashindano ni kuibua vipaji vya vijana mkoani Iringa,Kuonesha
uwezo wa vijana na kutengeneza ajira kwao,Kujenga
kizazi chenye afya bora na kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi,Kutoa burudani
kwa wakazi wa iringa kwa mchezo wa mpira
wa miguu,Kuwakutanisha vijana pamoja ili kuzungumza lugha moja ya kimichezo na
maendeleo,Kuwaepusha vijana na makundi au vijiwe visivyo faa na Kuhamasisha
michezo katika mkoa wa Iringa,kutimiza agizo la makamu wa raisi juu ya kufanya
mazoezi
“Sasa hapo utagundua kuwa jinsi
gani mashindano hayo yalivyo yanaumuhimu katika kukuza vipaji hapa mkoani kwa
ustawi wa soka letu la nchi hiii” alisema Malekela
Aidha Malekela alizitaja zawadi pamoja na vifaaa ambavyo
vitatolewa kwa timu shiriki
VIFAA
msimu wa mwaka huu wa 2018 Kupitia mdhamini
RITTA KABATI tunataraji kutoa vifaa vya
michezo kama ifuatavyo kwa timu shiriki.
Kifaa
|
Muhusika
|
idadi
|
Mipira ya
mazoezi
|
Timu shiriki
|
Mpira mmoja
(1)
|
Jezi za mechi
|
Timu shiriki
|
Jezi set 1
|
Jezi za
waamuzi
|
Waamuzi
|
Set 6
|
No comments:
Post a Comment