Msanii wa bongo fleva ambaye haishiwi vituko Harmorapa,
amefunguka na kusema Alikiba ni msanii ambaye amekosa mfano hapa Tanzania
kutokana kazi zake na namna ambavyo amekuwa akifanya mambo yake nje ya muziki.
Harmorapa amesema hayo siku chache baada ya Alikiba kudondoka
wino na kampuni ya usimamizi wa kazi za wasanii RockStar4000 na kuwa Mkurugenzi
wa muziki na vipaji wa kampuni hiyo, pia kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni ya
Rockstar4000 Music Entertainment Co & Rockstar Television.
"Katika vitu ambavyo tunatakiwa kujivunia ni kuwa na
wasanii ambao wanatangaza taifa letu mbele na kujivunia juhudi zao. Naimani
heshima, busara na juhudi ndiyo nyenzo pekee zilizowafanya wazungu kumwaga wino
na kumkaribisha Alikiba meza moja na kumkabidhi kampuni kubwa ya Rockstar4000
kuwa mmiliki mmoja wapo na Director" alisema Harmorapa.
Mbali na hapo Harmorapa aliwataka wasanii wengine kujifunza na
kujivunia uwepo wa Alikiba kwani amekuwa akiutendea haki muziki wa bongofleva
na kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania nje ya nchi.
"Wasanii wa Tanzania inabidi tujifunze na kujisifu kwa kuwa
na King Alikiba maana anautendea haki mziki wetu wa bongo fleva, hongera zangu
zizidi kutiririka kwa King wewe uliokosa mfano hapa bongo" alisisitiza
Harmorapa.
Harmorapa ni kati ya
wasanii ambao wamekuwa na mapenzi sana na Alikiba kwani mara kadhaa amekuwa
mstari wa mbele kuonyesha mapenzi yake hayo kwa msanii huyo na kuonyesha jinsi
gani anamkubali, kiasi cha kuhangaika sana japo aweze kufanya naye collabo,
Harmorapa alishawahi kusema uongozi wake unahangaika kuona kama wanaweza kupata
fursa ya kufanya kazi na Alikiba.
No comments:
Post a Comment