Ndege inayomilikiwa na
kampuni ya Safari Air Link ambayo ilikuwa ikitokea Arusha kuelekea Serengeti
mkoani Mara kwa ajili ya kuchukua abiria, ilianguka na kusababisha kifo cha mtu
mmoja ambaye ni rubani.
Ndege hiyo yenye uwezo wa
kubeba abiria watano ilianguka jana katika milima ya Monduli kijiji cha
Engalaon kilichopo wilaya ya Arumeru mpakani na wilaya ya Monduli huku chanzo
cha tukio hilo bado hakijajulikana.
Akithibitisha kutokea kwa
tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Omari
Mkumbo alisema kwamba ndege hiyo aina ya Cessina 206 yenye namba za usajili
5H-SAL 206 ilianza safari ya kutoka uwanja wa ndege wa Arusha jana muda wa saa
1:05 Asubuhi ikiwa na rubani pekee na muda wa saa 4:00 Asubuhi taarifa za
kuanguka ndege hiyo zilianza kusikika.
“Mara baada ya taarifa hiyo muda wa saa 6:30 Mchana ndege hiyo ilionekana na kubainika kuwepo kwa mwili wa mtu mmoja ambaye ni Rubani aliyejulikana kwa jina la David Mbale (25) mkazi wa Dar es saalam ambao umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru”. Alisema Kamanda Mkumbo, na kubainisha kuwa uchunguzi wa tukio hilo utafanywa na wataalamu ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

No comments:
Post a Comment