BAADA ya kugundulika makosa kwenye maneno yaliyoandikwa katika
ngao ya jamii ambayo Simba waliitwa jana, shirikisho la mpira wa miguu Tanzania
TFF limeomba radhi na kuahidi kuibadili ngao hiyo.
Hii
hapa taarifa ya shirikisho hilo.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
AGOSTI 24, 2017
KUHUSU NGAO YA JAMII
Neno SHIELD
limekosewa na kuandikwa SHEILD
Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF), linaomba radhi wanafamilia wote wa mpira wa miguu
kutokana na makosa ya maandishi yaliyoonekana kwenye utambulisho wa Ngao ya
Jamii iliyotolewa Jumatano Agosti 23, 2017.
Ngao hiyo ilitolewa mara baada ya mchezo uliokutanisha timu za Simba SC
na Yanga SC za Dar es Salaam kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa jijini. Katika mchezo
huo, Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya Yanga na kutwaa Ngao
hiyo.
Watanzania hususani wanafamilia ya mpira wa miguu popote pale, TFF
hatujapokea vizuri mwonekana wenye makosa kwenye Ngao hiyo ya Jamii kama
ambavyo wadau hawajapokea vema suala hili.
Kutokana na makosa hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, tayari amechukua
hatua za kinidhamu kwa watumishi waliohusika kadhalika kuwasiliana na uongozi
wa Simba SC kuirejesha Ngao hiyo ili kufanyiwa marekebisho yatakayobaki kwenye
kumbukumbu sahihi.
Hatutegemei tukio kama hili kujirudia tena.
No comments:
Post a Comment