Kampuni
ya Uber imeanzisha kampeni ya kuhamasisha inayotoa miongozo inayowahimiza
watumiaji wa programu hiyo kutumia fursa ya teknolojia ya kampuni hiyo
inayoiwezesha Uber kuimarisha usalama miongoni mwa wasafiri na madereva.
Miongozo hii ya usalama sasa inapatikana kwa watumiaji wake wote walioko jijini
Nairobi, Mombasa, Dar es Salaam, na Kampala.
Miongozo
hii ya usalama ni ushahidi wa juhudi za Uber za kubuni teknolojia rahisi na ya
uhakika, inayorahisisha shughuli za wasafiri na madereva sambamba na kuwalinda
wanapokuwa safarini.
Katika
miongozo hii, wasafiri wanaombwa wathibitishe namba za usajili za gari ili
wahakikishe zinafanana na gari lililo kwenye programu, kadhalika picha ya
dereva kabla ya kupanda gari. Aidha, madereva wamepewa mafunzo ya
usalama, mbali na kwamba wana namba ambazo wanaweza kupiga bure iwapo kuna
tatizo.
Meneja
Msimamizi wa Uber nchini Tanzania Bw. Alfred Msemo amenukuliwa akisema:
“Kampuni ya Uber imekuwa ikitoa usafiri salama na wa kutegemewa na
Watanzania kwa mwaka mmoja sasa. Watu wengi wanategemea Uber katika
mahitaji yao ya usafiri kila siku. Uber inatumia teknolojia kuhakikisha kuna
usalama katika huduma zetu kuanzia mwanzo hadi mwisho wa safari: kabla ya
msafiri kupanda gari, wakati wa safari, na baada ya kuwasili mahali anakoenda.”
Zana
hizi za usalama zinawataka wasafiri wasiondoke kwenye programu wakati wa safari
kwa sababu safari inafuatiliwa kwa kutumia mfumo wa GPS kuanzia mwanzo hadi
mwisho. Ufuatiliaji huu unawawezesha kuona barabara wanayotumia, mahali gari
lipo, na kujua iwapo dereva anatumia barabara sahihi. Programu ya Uber pia
inatumia kipengele kinachowawezesha wasafiri kutuma maelezo ya safari zao
mubashara kwa jamaa na marafiki, ikiwa ni pamoja na barabara wanayotumia na
muda wa kuwasili.
Mapema
mwaka huu, Uber ilichapisha miongozo ya jamii katika kanda ya Afrika Mashariki,
Makala yanayolenga kutoa mwongozo wa tabia ambazo wasafiri na madereva
wanapaswa kudumisha na jinsi ya kuchukuliana wao kwa wao wanapokuwa safarini.
Tazama
mikakati iliyo hapa chini ambayo wasafiri wanahimizwa kuzingatia:
Usaidizi wa Ndani ya Programu: Hii ni zana iliyoundwa ili iwasaidie wasafiri
kupata jibu haraka wanapouliza swali lolote. Msafiri anaweza kutumia mfumo wa
huduma kwa wateja kwa kuenda kwenye sehemu ya “Usaidizi’’ kwenye menyu, zana
hii inawasaidia wasafiri na madereva kueleza wasiwasi walionao wakati wa safari
na watapata majibu mara moja.
Kuonesha
Maelezo ya Safari: Teknolojia ya Uber
imefanikisha uwezo wa kufuatilia safari zote kwa kutumia mfumo wa GPS. Abiria
akiwa safarini anaweza kufuatilia safari yake katika programu sambamba na
kuwaambia jamaa zake Muda Atakaowasili (ETA). Teknolojia hii itawasaidia jamaa
na marafiki kufuatilia mahali alipo na wanaweza kufanya hivyo bila kutumia
programu ya Uber!
Jua
Safari Yako: Wasafiri wanahimizwa
watumie vipengele vya usalama vinavyopatikana katika programu, kumbuka kwamba
msafiri anaweza tu kuita usafiri wa Uber kwa kutumia programu ya Uber, kwa hiyo
watumiaji wasikubali madereva ambao wanajiitia kwamba wanafanya kazi na kampuni
ya Uber wawachukue.
Ni
muhimu wasafiri wawe wangalifu na wasitumie muda mwingi wakiwa wamesimama
wenyewe na simu zao mkononi wanapotaka kuita gari. Wanashauriwa kusubiria ndani
ya jengo mpaka programu iwaoneshe kwamba gari limewasili.
Mjue
Dereva Wako: Dereva akikubali safari,
msafiri anaweza kuona jina, picha, namba pleti, aina ya gari, na rangi ya gari.
Maelezo haya yote utayaona kwenye programu – kwenye ramani. Wasafiri wanaombwa
wahakikishe kwamba maelezo waliyoona kwenye programu yanawiana na maelezo ya
gari kabla ya kupanda.
Fuata Machale Yako: Wasafiri wanaombwa wahakikishe kwamba wanaelewa mazingira
yao wanapotumia Uber, ikitokea kwamba kuna kitu chochote wanachokishuku
wanaombwa watumie busara kufanya maamuzi yenye tija maishani mwao. Wawe
wangalifu wanapoonesha maelezo yao na wahakikishe kwamba wanathibitisha kwamba
dereva anayewaendesha ni yule waliyemwona kwenye programu, na kama wanahisi
kwamba wanahitaji usaidizi wa dharura, wanaombwa wawasiliane na meza yoyote ya
dharura iliyo karibu mara moja.
Toa Maoni: Wasafiri wanaombwa kutoa maoni kuhusu safari ilivyokuwa. Maoni haya
yanasaidia kuboresha wigo wa safari za Uber kwa kila mtumiaji, kudumisha huduma
za ubora wa hali ya juu na kuleta uwajibikaji. Kampuni ya Uber ina kikosi maalum kinachotoa huduma kwa wateja
wakati wowote kote ulimwenguni kinachopitia maoni na kuchukua hatua stahiki
kutokana na ripoti na mienendo inayokiuka Miongozo ya Jamii ya Uber.
No comments:
Post a Comment