Kampuni ya Uber nchini Tanzania imetangaza zana mpya maarufu kama
“Kuchati Ndani ya Programu” inayowawezesha madereva na wasafiri kuandikiana
ujumbe kwa kutumia programu hiyo bila malipo.
Kinyume na hapo awali ambapo madereva na wasafiri wangetumia
Ujumbe Mfupi (SMS) au kupiga simu, zana hii inaleta unafuu kwa madereva na
wasafiri hivyo basi kuwapunguzia kadhia ya gharama za kupiga simu sambamba na
kuharakisha mawasiliano bila kuondoka kwenye programu ya Uber.
Maboresho haya ni juhudi endelevu za Uber na yanalenga kuimarisha
wigo wa wasafiri na madereva wanapotumia programu ya Uber.
Zana hii mpya ni rahisi sana kuitumia. Msafiri anapoita gari, kuna
kitufe cha ‘Kuwasiliana’ kwenye menyu inayoonekana chini ya skrini. Wasafiri
wanaweza kuwaandikia ujumbe madereva, na madereva vivyo hivyo. Ujumbe utaonesha
kwamba umepokelewa baada ya kuutuma.
Kwa upande mwingine, madereva watakiri kwamba wamesoma ujumbe kwa
kugusa kwenye programu ya Uber ili watume ujumbe wa ‘bomba’. Ili
wasijichanganye barabarani. Aidha wasafiri na madereva wanaweza kuona kama
ujumbe wao waliotuma umesomwa.
Meneja Msimamizi wa Uber nchini Tanzania Bw. Alfred Msemo amehoji
kwamba, “Kila safari nzuri huanza pale msafiri anapochukuliwa kwa gari, kwa
hiyo tunajituma kutafuta mbinu za kumchukua msafiri bila usumbufu wowote kwa
msafiri au dereva. Kipengele hiki cha Kuchati kitakuwa afueni kwa wasafiri na
madereva wanapotaka kuwasiliana ili kusaidiana kutafuta mwafaka wa changamoto
za safari kama vile, kufungwa kwa barabara au kutoa maelezo ya mahali walipo.”
Kadhalika, kipengele hiki kinatoa njia mbadala ya wasafiri na
madereva kupiga simu wanapotaka kuwasiliana. Hata hivyo, ili mtu atumie
kipengele hiki anatakiwa awe anatumia toleo la sasa la program ya Uber.
“Huu ni mwanzo tu wa mchakato wa kuimarisha huduma za kutuma
ujumbe moja kwa moja kwenye programu ili kufanikisha wigo wa mawasiliano yasiyo
na changamoto kwa wateja wetu, na kuwasaidia kuwasiliana katika ulimwengu wa
utandawazi na ulimwengu halisi” amenukuliwa Bw. Msemo.
No comments:
Post a Comment