Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro
Nyalandu jana alikuwa jijini Nairobi nchini Kenya ambapo alikwenda
kuchukua dawa kwa ajili ya mgonjwa Samson Mwanga ambaye alipasuka mshipa
wa kichwa ametangaza kuwa mgonjwa huyo amepoteza maisha alfajiri ya
leo.
Nyarandu amesema kuwa mgonjwa huyo
Samson Mwanga amefariki dunia alfajiri ya leo akiwa katika Hospitali ya
rufaa ya KCMC iliyopo Moshi mkoani Kilimanjaro.
"Nilikuwa hospitali ya KCMC, Moshi saa
7:00 usiku kuamkia leo kupeleka dawa (Intravenous Immunoglobulin)
nilizozitoa Nairobi Hospital na kuzisafirisha usiku kwa ajili ya
kuendelea kumtibu mgonjwa Samson Mwanga tuliyemrusha kwa ndege toka
Hydom Hospital Jumanne iliyopita. Kwa bahati mbaya sana, tumempoteza
Samson alfajiri majira ya 11:00 asubuhi" alisema Nyalandu
Aidha Mbunge huyo wa Singida Kaskazini
ametoa shukrani zake kwa madaktari wa KCMC kwa kila walichoweza kufanya
ili kuweza kuokoa maisha ya Samson mpaka pale umauti ulipomkuta alfajiri
ya leo.
Septemba 26, 2017 Lazaro Nyalandu
aliweza kufanikisha safari ya Samson kutoka katika hospitali ya Hyadom
na kumpeleka Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Kilimanjaro kwa dharura
kutokana na mgonjwa huyo kupasuka mshipa wa kichwa hivyo alipelekwa KCMC
kwa matibabu zaidi lakini leo amepoteza maisha akiwa bado anapatiwa
matibabu.
Bwana ametoa, na Bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe.
No comments:
Post a Comment