Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli ameahidi kuwafukuza kazi Wakurugenzi wa
halmashauri wanne kwa ulevi wa pombe pindi wawapo makazini.
Rais Magufuli amesema hayo alipokuwa
kwenye Mkutano wa 33 wa Jumuiya Ya Tawala za Mitaa (ALAT) ambao
uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam
na kusema amepata taarifa kuwa wapo Wakurugenzi kadhaa ambaio ni walevi
na kudai wasipobadilika ndani ya muda mfupi atawafukuza kazi.
"Nimepata taarifa ya Wakurugenzi kama
wawili watatu hivi ni walevi sana, nawaambia hao wataondoka kama upo
hapa Mkurugenzi halafu ni mlevi ukajirekebishe haraka sana, kabla sijaja
huko ili angalau uonekane umebadilika" alisema Rais Magufuli.
Mbali na hilo Rais Magufuli aliwataka
viongozi hao kwenda kumaliza migogoro mbalimbali ndani ya halmashauri
zao na mivutano isiyokuwa na msingi na kusema kuwa vyama vya siasa si
adui bali adui wa kwanza wa serikali yake ni watu wanaokuja kuiba
maliasili za Tanzania.
"Haipendezi kuwa na makundi muyamalize
makundi hayo kwenye manispaa, tunajenga nyumba moja adui yetu siyo vyama
tunachelewa sana, adui yetu ni wale wanaotuibia nasema mkamalize hayo
makundi huko, najua tofauti lazima zitakuwepo lakini kwenye masuala ya
kazi lazima tushikamane kwa maslahi ya Watanzania, mkawaimize Watanzania
kufanya mambo ya maendeleo" alisisitiza Rais Magufuli
No comments:
Post a Comment