Kampuni ya Uber imezindua bidhaa mpya ya kuwasaidia madereva katika shughuli zao - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, November 2, 2017

Kampuni ya Uber imezindua bidhaa mpya ya kuwasaidia madereva katika shughuli zao


Kampuni ya Uber ina furaha kuwatangazia madereva wake wote kwamba imezindua vipengele vipya vyenye uwezo mkubwa vitakavyowasaidia madereva kutoka kanda ya Afrika Mashariki kuwa na uhuru wa kuchagua maeneo, muda na namna wangependa kuendesha gari kwenye mfumo wa Uber. Halikadhalika Uber imeongeza mara dufu uwezo wa programu yake na kuifanyia maboresho makubwa.  

Vipengele hivi vipya vinakuja baada ya zana ya Kuchati Ndani ya Programu Iliyozinduliwa hivi karibuni, kipengele kinachowasaidia madereva na wasafiri kuwasiliana kwa kutumia programu ya Uber bila kuonesha namba zao za simu wanapotaka kuwasiliana.

Meneja Msimamizi wa Uber Nchini Tanzania, Alfred Msemo, anaelezea, "Siku zote sis hufanyia kazi maoni ya madereva wetu ambayo hutusaidia katika kuboresha na kuimarisha wigo wa madereva wanaotumia mfumo wetu. Madereva wanaotumia mifumo yetu wameeleza wazi kuhusu kile wanachotaka na tumefanyia kazi maoni yao, kwa hiyo tutazindua bidhaa ambazo zitasaidia kutafuta mwafaka katika sehemu tatu kuu: kuwapa madereva uhuru zaidi hasa namna wangependa kutumia mfumo wa Uber, kutumia teknnolojia kuwaondoleaa kero zozote wanazopata kazini, pamoja na kuimarisha usalama.”

Kampuni ya Uber itaanza kwa kuzindua bidhaa kadhaa ambazo madereva wameomba:
  •  Kuonesha Safari Yangu ya Dereva: Tayari Uber ina njia ambayo msafiri anaweza kuwaonesha watu wanaotaka alipofika kwenye safari yao yake, sasa kipengele cha Kuonesha Safari Yangu kinatoa nafasi kwa madereva kuonesha watu wa karibu maelezo ya safari yao, bila kuingilia faragha ya msafiri au kutoa taarifa ya kibinafsi au vituo vya kuchukua na kushusha abiria.
  •  Kituo na Muda wa Kuwasili: Sasa madereva wanaweza kuweka muda wanaotaka kuwasili mahali wanakoenda wakati wowote kwa kutumia kipengele cha Muda wa Kuwasili. Madereva wakiweka kituo na muda wa kuwasili, wanapoendelea na shughuli zao za kawaida programu itawakumbusha muda wa kuanza safari ukifika. Muda ukifika wataunganishwa na msafiri aliyeita gari kwenye barabara hiyo. Kipengele hiki kinawapa uhuru zaidi wa kujisimamia sambamba na kupata pesa zaidi wanapokuwa njiani kuelekea kituo wanachotaka.
  •  Arifa ya safari ndefu: Madereva watapata taarifa mapema itakayowajulisha kuhusu safari ya mwendo mrefu, hii ina maana kwamba madereva watajua mapema ikitokea kwamba safari itachukua dakika 45 au zaidi, ili wafanye maandalizi ya kutosha.
  •  Kulinda Ukadiriaji: Wakati mwingine wasafiri wanaweza kukadiria safari vibaya kutokana na sababu ambazo sio kosa la dereva kama vile hitlafu kwenye programu ya Uber. Sera mpya ya kumkadiria dereva, ukadiriaji wa aina hii hautajumuishwa kwenye jumla ya ukadiriaji wa dereva. Bado kampuni ya Uber itandelea kupokea maoni yatakayosaidia kuboresha huduma zake lakini hayataathiri wastani wa ukadiriaji wa dereva.
  • Kitufe cha 'Hapana': Kipengele hiki kinawapa madereva uhuru wa kukataa safari bila hofu ya kwamba itaathiri mapato yao. Kwa sasa, madereva wanaweza kuthibitisha na kukubali safari au wasubirie muda wa ombi la usafiri uishe. Kipengele hiki kipya, cha kitufe cha 'hapana', kinawapa madereva uwezo wa kukataa safari mara moja - ni habari njema kwa wasafiri pia kwa sababu ombi litatumwa kwa dereva mwingine haraka hivyo hatapoteza muda mwingi akisubiria gari.

Ni nini tafsiri yake kwa madereva? Msemo anafafanua, “Fatuma Mdee anapofungua pprogramu na kuanza kukubali maombi ya wasafiri, anaweza kutumia kipengele cha “Onesha Safari Yangu” kumtumia mume wake maelezo ya safari yake. Maelezo haya ni kama vile mahali alikofika kwenye ramani. Ana uwezo wa kuanza kumwonesha mume wake na watu wengine lakini anaweza pia kuacha kuwaonesha maelezo ya safari yake muda wowote, na wanaweza kufuatilia mahali amefika bila ugumu wowote kwenye ramani kwa kutumia maelezo yake ya namba ya simu na namba pleti ya gari. ”

"Au kwa mfano, dereva Omar Mohammed, ambaye ni baba wa watoto watatu na anatumia programu ya Uber kumpa uhuru wa kusimamia maisha yake. Kitufe hiki kipya cha "Hapana", sasa kinawapa madereva kama Omar uhuru zaidi wa kusimamia safari kwa sababu kipengele hiki kinampa uwezo wa kukataa safari mara moja bila wasiwasi wowote wa mapato yake kupungua. Hii ni habari njema kwa wasafiri pia kwa sbabu ombi la usaifiri litatumwa moja kwa moja kwenda kwa dereva mwingine bila kupoteza muda wowote.

"Tunajituma kila siku kutumia uwezo wetu wa teknolojia na ofa zetu za madereva ili kuwajengea madereva mazingira rafiki na wafurahie kazi yao wanapotumia mfumo wa Uber. Tunaamini kwamba vipengele hivi vitaimarisha sio tu wigo wa madereva bali maisha yo pia. "Amehitimisha Bw. Msemo.

Lakini huu ni mwanzo tu - tumekusudia kuyapa kipaumbele maslahi ya dereva katika mkakati wa Uber, Uber itaendelea kujituma ili kuimarisha wigo wa madereva wanaotumia programu yetu. Maboresho haya si ya vipengele tu - ni sehemu ya mkakati endelevu, na Uber ina furaha kubwa kutumia uwezo wake wa kiteknolojia ili kuimairsha na kubadilisha wigo wa madereva 1,000 wanaotumia mfumo wa Uber kila wiki.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages