TUME
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa maandalizi ya vifaa kwa ajili
ya uchaguzi mdogo wa madiwani unaofanyika katika kata 43 yamekamilika na
awamu ya pili ya vifaa vitaanza kusafirishwa leo Ijumaa kwenda katika
kata husika.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa NEC Kailima Ramadhani, alisema kwamba vifaa
vitakavyosafirishwa kuanzia kesho ni maalumu kwa ajili ya kutoa mafunzo
kwa wasimamizi wa vituo, makarani waongozaji pamoja na mfano wa
karatasi za kupigia kura.
Alisema
awamu ya kwanza ya kusafirisha vifaa ulifanywa na tume wakati wa
mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi ambayo yalifanyika mjini Dodoma
ambavyo vilitumika wakati wa uteuizi wa wagombea udiwani katika kata
zote.
“Napenda
kuwahakikishia umma kwamba tume imejipanga vizuri kwa ajili ya uchaguzi
huu na maandalizi ya kupeleka vifaa katika husika yako vizuri na awamu
ya pili ya upelekaji wa vifaa itapaelekwa kesho (leo),”alisema
Ramadhani.
Alisema
awamu ya tatu ya usafirishaji wa vifaa itahusisha vifaa vichache
ambavyo ni karatasi za kupigia kura pamoja na fomu za kutangazia
washindi ngazi ya kituo na ngazi ya kata.
Naye
Mkurugenzi wa Manunuzi, Ugavi na Logistiki wa NEC Eliud Njaila, alisema
kwamba NEC imepeleka vifaa vya kutosha katika vituo vyote 893
vilivyoko katika kata 43 na hakutakuwa na upungufu wowote.
Alisema
kwamba katika awamu ya pili ya upelekaji wa vifaa, wameweka na mfano wa
karatasi za kupigia kura ili wadau ambavyo ni vyama vya siasa
vijiridhishe kuhusu karatasi hivyo zitakavyokuwa pamoja na kufanya
uhakiki wa majina wa wagombea wao.
“Tunaamini
kwamba vyama vya siasa vitahakiki majina ya wagombea wao kwa kila kata
ili kama kuna masahihisho wayalete mapema na NEC iweze kufanya
masahihisho haraka wakati wa kuchapa karatasi halisi za kupigia kura,”
alisema Njaila.
Njaila
pia aliwataka wasimamizi wa uchaguzi wa wilaya kuwatumia maafisa
boharia katika kupokea na kutunza vifaa hivyo. Alisema wataalamu hao pia
ndio watumike pia kusafirisha vifaa hivyo kwa kuwa wao wana ujuzi wa
namna ya kutunza na kugawa vifaa.
Aliongeza
kuwa iwapo wasimamizi wa uchaguzi watawatumia maafisa ugavi ni wazi
kuwa hakutakuwa na malalamiko ya kupungua kwa vifaa katika vituo vya
kupigia kura.
Naye
Ofisa Uchaguzi wa NEC Sada Kangeta, alisema kuwa tayari wameshafanya
uhakiki wa vifaa vya uchaguzi na wamejiridhisha kuwa vifaa vyote vipo
kama inavyopaswa na kwamba hatua itakayofuata ni usafirishaji wa vifaa
hivyo katika maeneo husika.
Aidha
aliwataka wapiga kura wote wa maeneo husika, wagombea wa vyama vyote
vya siasa na wadau wa siasa kutokuwa na hofu juu ya vifaa hivyo kwa
madai kuwa hakuna upungufu wowote utakaojitokeza.
No comments:
Post a Comment