MEYA WA KINONDONI ABORESHA SEKTA YA AFYA KATA YA KIGOGO - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, December 14, 2017

MEYA WA KINONDONI ABORESHA SEKTA YA AFYA KATA YA KIGOGO

Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa hati ya jengo la kituo cha Afya kata ya Kigogo jijini Dar es Salaam leo hii.

Naibu Meya ambaye pia ni Diwani wa Kata  ya Kigogo Mangalu Mnyama (kulia) akizungumza kwa furaha na kutoa shukrani kwa wote waliofanikisha hatua zote za kununuliwa kwa jengo hilo.

akikabidhi hati ya Jengo hilo kwa Meya wa Kinondoni.

Mganga mkuu wa Manispaa ya kinondoni Dk. Festo Dugange akiungumza.



Viongozi mbalimbali wa serikali za mitaa waliofika katika.zoezi hill la kukabidhiwa jengo kwa ajili ya ahanati
 Hili ndilo jengo ambalo linatarajiwa kuwa kituo hicho

Meya wa Manispaa ya Kinondoni   Benjamin Sitta amemwomba mganga mkuu kuharakisha ukarabati wa Jengo lililonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kituo cha  Afya  cha Kigogo jijini  Dar es Salaam, litakalogharimu kiasi cha shilingi milioni 46 kwa lengo la kusaidia matibabu kwa wananchi haraka ipasavyo.

Sitta ameyasema hayo leo katika hafla ya kukabidhiwa hati ya  Jengo hilo ambalo kwa sasa ni  kituo  cha Afya  Manispaa ya konondoni kata ya kigogo, lililonunuliwa na serikali kutoka  Dogodogo Center Street Children Trust(Caring for  our Childen)  lililogharimu kiasi cha shilingi milioni 400.
Amesema mahitaji katika sekta ya afya ni mkubwa sana na hivyo serikali inajtahidi kupunguza bajeti kwenye vitu vingine inawekeza kwenye mambo kama haya ya kijamii kwani wananchi wanauhitaji mkubwa katika sekta ya Afya .

"Mahitaji ya wananchi wetu kwenye sekta ya afya bado ni makubwa sana ,lakini kigumu zaidi kwenye manispaa yetu ya Kinondoni,Na kigogo ikiwa na kituo cha afya itahudumia watu wengi kutoka sehemu tofauti tofauti na tunayafanya haya kwa wananchi wetu wote,katika kuwatekelezea mahitaji yenu muhimu ambapo afya ni namba moja kwa jamii.Amesema Meya wa Kinondoni.


Aidha amesema   katika  manispaa hiyo wanategemea kila mtaa uwe na Zahanati na kila Kata kuwe na kituo cha afya ili kufanikisha hayo amesema wanategemea kujenga hospitali ya kisasa Magwipande lengo likiwa ni kupunguza msongamano katika hospitali ya Mwananyamala,sambamba na kujenga hospitali ya Apolo India itakayohudumia wagonjwa wanaokwenda kutibiwa huko.

"Tumefanya jambo kubwa sana,ni mategemeo yetu kila Mtaa uwe na Zahanati na kila kata kuweze kuwa na  Kituo cha Afya, ingawa tuna upungufu wa Zahanati  84, pamoja na vituo vya afya 18 na tumeanza mazungumzo  ya kujenga hospitali ya Apolo ya India yetu itakayosaidia kupunguza wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje na kuweza kutbiwa hapa hapa nchini  na pia  tunatarajia kujenga hospitali ya kisasa kabisa Mgwipande katika manispaa yetu itakayopunguza msongamano katika hospitali yetu ya Mwananyamala" Amesema Sitta.

Kwa upande wake Naibu Meya ambaye pia ni Diwani kata ya kigogo Mangalu Manyama,ameishukuru Serikali katika kufanikisha kununuliwa kwa Jengo hilo ambapo litakarabatiwa na kuwasaidia wakazi wa kata ya kigogo kupata matibabu katika kituo hicho.

Mganga mkuu wa manispaa ya Kinondoni Dk. Festo Dugange amesema katika halmashauri hiyo inatekeleza Adhima ya serikali kujenga Zahanati pamoja na Vitio vya Afya ili kuhakikisha huduma za afya zinaboreka katika jamii ambapo majengo waliyonunua kutoka Dogodogo Center itasidia wananchi kupata huduma kwa haraka Zaidi kutoka katika kituo cha Afya kwani Katika Zahanati ya kigogo inahudumia watu 66,654 kutokana na ufinyu wa majengo ya  huduma za afya.


”Majengo haya na eneo hili lililonunuliwa kutoka Dogodogo Center itasaidia sana kupunguza msongamano wa Wagonjwa katika Zahanati ya KIgogo kimsingi Zahanati inatakiwa isihudumie wagonjwa zaidi ya 5,000 lakini zahanati yetu inawahudumia wakazi wapatao 66,654 zaidi ya mara kumi na mbili ya uwezo wa zahanati" Amesema Dk. Dugange.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages