Saturday, January 27, 2018

Home
KITAIFA
RC MAKONDA ATOKWA NA CHOZI, NI BAADA YA KUJIONEA MAISHA YA WASTAAFU WALIODHULUMIWA NYUMBA
RC MAKONDA ATOKWA NA CHOZI, NI BAADA YA KUJIONEA MAISHA YA WASTAAFU WALIODHULUMIWA NYUMBA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akimfariji Bi. Stella Bejumula mstaafu alietapeliwa nyumba yake
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo
ametembelea na kutoa pole kwa Familia ya Wastaafu ya Bwana Edward Bejumula na Bi. Stella Bejumula walioteseka kwa Miaka Sita bila Makazi baada ya kudhulumiwa Nyumba yao ambapo ameahidi kulivalia njuga suala hilo kuhakikisha haki inatendeka bila kuvunja sheria.
RC Makonda amewatembelea wastaafu hao na kuwapatia Masada wa vitu mbalimbali ikiwemo Mchele, Unga, Sabuni, Ngano, Mafuta,Nyama,Viazi, Maharage, Sukari, Vitunguu, Ndizi, Nyanya kwaajili ya matumizi ya nyumbani baada ya familia hiyo kupoteza Mali zote.
Stori ya wastaafu hao kudhulumiwa Nyumba waliyojenga baada ya kufanya kazi kwa Miaka 34 imemgusa RC Makonda hadi kujikuta anashindwa kuvumilia na kutokwa na machozi kutokana na namna inavyouzunisha kuona mnyonge anajituma kwenye kazi na kufanikiwa kujenga nyumba alafu anatokea mtu anatokea mtu anamdhulumu Mali yake.
Makonda amesema kazi ya kutafuta haki ya wastaafu hao inaanza Mara moja kwa kuwahoji watu wote waliohusika na sakata hilo wakiwemo Benki, Muuzaji wa nyumba, Mnunuzi, kampuni ya udalali ya Majembe, Watu wa Mahakama na watu wa ardhi.
Kwa sasa wastaafu hao wanaishi kwenye nyumba ya mfadhili mmoja aliejitolea kusitiri familia hiyo ambapo RC Makonda amemshukuru kwa moyo alioonyesha.
Kwa upande wao Wastaafu waliodhulumiwa Mali zao wamefurahia kitendo cha RC Makonda kuona taarifa zao kwenye vyombo vya habari kisha kuwatembelea na kuwasikiliza kitendo kilichowafariji na wanaamini kwa utendajikazi wa RC Makonda wanapata haki yao.
Aidha wamemshukuru RC Makonda kwa kitendo cha kuwapelekea Chakula kwakuwa wameishi maisha ya tabu hadi kukosa vitu vya ndani ikiwemo vyakula ambapo wamemuombea kwa Mungu azidi kumpa maarifa ya kuwasaidia wananchi wanyonge.
Bwana Edward Bejumula akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa jinsi walivyotapeliwa nyumba hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akikabidhi vyakula na mahitaji mbalimbaya kibinadamu alipokwenda kuwatembelea wastaafu hao waliotapeliwa nyumba
Hii ndio nyumba waliotapeliwa wastaafu hao
Tags
# KITAIFA
Share This
About kilole mzee
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
MAGAZETI YA JUMAPILI LEO JANUARY 28, 2018
Older Article
RC MAKONDA: Azindua Uezekaji Paa Ofisi za Walimu shule ya Msingi Mapinduzi Kinondoni
WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MAKOREMO-MGONGORO
Hassani MakeroMar 12, 2025"Stori za Afya za Wanawake wa Tanzania zina thamani kwetu", Absa Bank
Hassani MakeroMar 12, 2025HALMASHAURI KUU YA CCM YAPENDEKEZA MAREKEBISHO YA KANUNI ZA UTEUZI WA WAGOMBEA UONGOZI
Hassani MakeroMar 11, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment