UVCCM MKOANI TANGA YAWEKA KAMBI UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, September 18, 2018

UVCCM MKOANI TANGA YAWEKA KAMBI UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoani Tanga, Omari Mwanga akizungumza wakati wa  ghafla ya uzinduzi wa kambi ya Vijana wa chama hicho kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Muheza ambapo mgeni rasmi Mbunge wa Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu alisema ushirikiano uliofanywa na vijana hao wa kushiriki katika mradi mkubwa kama huo ni jambo la kuigwa nchi nzima.
 Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa Tanga Zawadi Nyambo akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alisema mpango kazi wa miaka mitano 2017-2022 ambao uliwasilishwa katika Mkutano Mkuu wa UVCCM Mkoa ukiwa na lengo la kuanzisha makambi katika ngazi mbalimbali.
 Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akizungumza 


 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Muheza Like Gugu akizungumza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajabu na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Tanga Omari Mwanga kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo.
 Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Juliaus Mgeni akitoa taarifa ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo.
VIJANA wa UVCCM Mkoani Tanga wakiendelea na ujenzi 
 Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu katikati akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Tanga Omari Mwanga.
 MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akivalisha taji mara baada ya kuwasili kwenye kambi hiyo ya vijana.
 MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu katikati akimaliza kukagua gwaride la vijana mara baada ya kuwasili eneo la mradi wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Muheza Lusanga kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoani Tanga Omari Mwanga.
 MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu katikati akimsikiliza kwa umakini Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Like Gugu.
 MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu katikati akiwa na Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Tanga kulia Omari Mwanga wakiangalia lori lililoleta saruji kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza inayojengwa eneo la Lusanga.
 MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu katika akiwa na Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Tanga Omari Mwanga wakipiga makofi wakati vijana wakiimba nyimbo mbalimbali.

UJENZI wa Hospitali ya wilaya ya Muheza mkoani Tanga umeanza kushika kasi baada ya vijana 300 wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoani Tanga kuungana kwa pamoja kuweka kambi maalumu kwa ajili ya kujitolea kwenye mradi huo.

Vijana hao wa UVCCM Mkoani Tanga kutoka wilaya zote walianza kambi hiyo Septemba 10 mwaka huu eneo la Lusanga kunapojengwa hospitali hiyo walianza kujitolea na wataalamu katika utekelezaji wa mradi huo kwa awamu ya kwanza kujenga majengo ya utawala,wodi ya wanawake,wodi ya watoto,jengo la maabara,jengo la utakasaji vifaa na jengo la dharura ambayo yatagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 3.

Akizungumza katika ghafla ya uzinduzi wa kambi hiyo mgeni rasmi Mbunge wa Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu alisema ushirikiano uliofanywa na vijana hao wa kushiriki katika mradi mkubwa kama huo ni jambo la kuigwa nchi nzima.

Balozi Adadi alisema ipo miradi mingi ambayo inaendelea kutekelezwa katika Halmashauri mbalimbali na ikiwa watawatumia vijana hao wa chama ni wazi wanaweza kujengwa kiuzalendo zaidi na kusaidia kuharikishautekelezaji wake.

Alisema atahakikisha vijana hao wanapatiwa vifaa muhimu vya kujikingapindi wawapo katika shughuli hiyo ya ujenzi na wanapatiwa chakula chakutosha na mahitaji mengine muhimu ili azma yao ya kuyafikisha majengo hayo uwasa wa lenta Sept 25 iweze kutimia.

Kwa Upande wa Mkuu wa Wilaya Muheza Mhandisi Hajat Mwanasha Tumbo alisema azimio ni kupata Hospitali ya wilaya hivyo waliona vijana watumike ili kuwajengea uzalendo na kufanya hivyo Serikali inaweza kufikia malengo yake.

Tumbo alisema jambo hilo liwe chachu kwa chama na Serikali kwenye azma ya kutatua kero za wananchi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo haitekelezwi kwa wakati na kusababisha wananchi kuendelea kuteseka.

“Tunahaja ya kuwatumia vijana hawa sasa hasa katika miradi yetu ya kimaendeleo na si kuwaacha tu na tukifanya hivi tutakuwa tunawajenga kiuzalendo wa kujua chama chao na Serikali nini wanachokifanya kwa
ajili ya wananchi wake”Alisema Tumbo.

Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama hicho Mkoa Tanga Zawadi Nyambo alisema mpango kazi wa miaka mitano 2017-2022 ambao uliwasilishwa katika Mkutano Mkuu wa UVCCM Mkoa ukiwa na lengo la kuanzisha makambi katika ngazi mbalimbali.

Nyambo alisema nguvu itakayotumika kupitia vijana hao ipo imani kubwa ya kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kitatumika katika shughuli zingine za maendeleo ya kijamii na kuieleza jamii umoja wa vijana hao sio siasa pekee bali ni pamoja na ujenzi wa Taifa.

Katibu huyo alisema wameazimia kuwatumia vijana kuwajenga katika suala zima la uzalendo kama nguvu kazi katika miradi mbalimbali inayoanzishwa na Serikali”Alisema.

Awali akisoma taarifa fupi mbele ya mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Juliaus Mgeni alisema Wilaya hiyo tangu ianzishwe miaka 45 iliyopita haina Hospitali ya Wilaya na kuitegemea Hospitali 1 ya Teule inayomilikiwa na Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga.

Alisema Hospitali inazidiwa uwezo kwa sasa mabpo uwezo wake ni kuhudiumia watu 1,500 kwa siku hivyo huduma za rufaa ikijumuisha wagonjwa wenye hali mbaya za kiafya toka vituo vya huduma za msingi wanalazimka kusafirihwa umbali wa km 72 hadi Hospitali ya Rufaa ya Bombo Mkoani Tanga.

Mgeni alisema Hospitali hiyo inatarajiwa kugharimu kiasi cha zaidi ya shili bilini 11 hadi kumalizika kwake ambapo unategemewa kutekelezwa kwa kipindi cha mika mitatu kuanzia 2017/18 -2019/2020 na itategemea upatikanaji wa fedha.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages