Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania (BBT) Abdi
Mohamedi,(kushoto) akikabidhi msaada wa vitabu
kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mshana katika hafla ambayo benki hiyo ilitoa msaada wa vitabu katika
shule za msingi
Manispaa ya Ilala, Dar es
Salaam jana, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika shuleni hapo
. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Sophia Mjema
Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya Barclays Tanzania (BBT) Abdi
Mohamedi,(kushoto) akikabidhi msaada wa vitabu
kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi
Gogo, Simon Mdendemi, katika hafla ambayo Barclays ilitoa msaada wa vitabu
katika shule za msingi tano za Manispaa ya Ilala, wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika shule ya Msingi
Uhuru Mchanganyiko jijini Dar es Salaam hapo . Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya
ya Ilala, Sophia Mjema.
Mkuu wa
Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (katikati), akikabidhi msaada wa
vitabu vilivyotolewa na Benki ya Barclays
Tanzania kwa Mwalimu Mkuu wa
Shule ya Msingi Mafanikio, Kandidus Ndiwu, katika hafla ambayo Barclays ilitoa
msaada wa vitabu kwa shule za msingi za Manispaa ya Ilala iliyofanyika katika Shule ya
Msingi Uhuru Mchanganyiko . Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania (BBT) Abdi Mohamedi na wengine wanaoshuhudia ni
baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo na
baadhi ya viongozi wa kamati ya shule.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania (BBT) Abdi
Mohamedi (kushoto), akikabidhi msaada wa vitabu
kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi
Kiyombo Magreth Ng'ombo, katika hafla ya kutoa msaada wa vitabu kwa shule za msingi za Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam
iliyofanyika katika Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko jijini hapo
jana. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (wa tatu
kulia) na wengine ni baadhi ya
wanafunzi wa shule hiyo na uongozi wakamati ya shule.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akikabidhi msaada
wa
vitabu vilivyotolewa na Benki ya Barclays kwa
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi
Yangeyange, Abraham Gabriel, katika hafla ya kutoa msaada wa vitabu kwa shule za msingi Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam iliyofanyika
katika Shule ya Uhuru Mchanganyiko jijini humo jana. Kushoto anayeshhudia
ni ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania (BBT) Abdi Mohamedi, na
wengine ni baadhi ya wanafunzi wa
shule hiyo na baadhi ya viongozi wa kamati ya
shule.
Mkuu wa Wilaya ya Ialala, Sophia Mjema (kushoto),
akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Barclays Tanzania katika hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment