Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018 mkoani humo. (Picha Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo).
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018 mkoani humo.
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mhe Sarah Chiwamba, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe Christopher Ngubiagai wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018 mkoani humo.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe kumsimamisha kazi mtumishi George Mboje na kumuondoa kwenye timu ya Operesheni Korosho.
Pamoja na kumundoa kwenye timu hiyo pia Katibu Mkuu ametakiwa kumuondoa kwenye Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko."Katibu Mkuu, nataka umuondoe huyu George kwenye hii timu na pia sitaki kumuona kwenye Bodi na Taasisi yoyote katika Wizara ya Kilimo" Alisisitiza Mhe Hasunga .
Mhe Hasunga ametoa agizo hilo leo tarehe 4 Disemba 2018 wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha Watendaji wa timu ya Oparesheni korosho kilichofanyika katika ukumbi wa CBT Mkoani Lindi na wakati wa kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018.
George Mboja ambaye yupo kwenye timu ya Oparesheni Korosho akiwakilisha Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko anatuhumiwa kwa Utovu wa nidhamu sambamba na kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo wakati wa Oparesheni Korosho inayoendelea nchini.Aidha, Waziri Hasunga amewahakikishia watendaji hao kuwa serikali ina fedha za kutosha kuwalipa wakulima wa Korosho lakini lazima wakulima wote wahakikiwe ili kujiridhisha kwamba anayelipwa ni mkulima wa mwisho na sio wafanyabiashara maarufu kama Kangomba.
Akizungumzia hatua iliyofikiwa na serikali kuhusu malipo ya wakulima wa korosho, alisema hadi kufikia Jana tarehe 3 Disemba 2018 uhakiki ulikwishafanyika kwenye vyama 220 kati ya vyama 504 vilivyopo katika Mkoa wa Mtwara, Lindi na Ruvuma na kati ya vyama 617 vinavyojihusisha na Korosho nchini.
Alisema kati ya vyama hivyo vilivyokwisha hakikiwa ni vyama 181 ndivyo ambavyo tayari vimelipwa fedha zao huku Bilioni 41.8 zikiwa zimelipwa.Aliongeza kuwa wakati zoezi hilo linaanza serikali ilikuwa inalipa Bilioni Moja kwa siku lakini kwa sasa utaratibu uliowekwa ni kulipa kati ya Bilioni 5 mpaka 10 kwa siku.
Katika taarifa yake Waziri Hasunga amesema kuwa jumla ya wakulima 40,208 wamekwishalipwa fedha zao.Mhe Hasunga aliongeza kuwa serikali imeamua kuwalipa wabebaji na wapakiaji wa mizigo kwenye maghala sambamba na kuanza kuwalipa malipo ya awali wasafirishaji kutoka kwenye vyama vya msingi kwenda kwenye vyama vikuu.
Kuhusu swala la magunia Waziri Hasunga alisema kuwa serikali imeamua kuyalipa magunia yote ili kurahisisha uhifadhi wa Korosho.
No comments:
Post a Comment