Paulo Dybala na mpenzi wake, Orina wakutwa na Virusi vya Corona - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, March 22, 2020

Paulo Dybala na mpenzi wake, Orina wakutwa na Virusi vya Corona

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Juventus ya nchini Italia, Paul Dybala amethibitisha yeye na mpenzi wake, Oriana kukutwa na maambukizi ya Virusi vya ugonjwa wa Corona baada ya kufanyiwa vipimo.
Dybala amesema yeye na mpenzi wake Oriana Sabatini ambaye ni MwanaMitindo wa Argentina wamekutwa na maambukizi ya Virusi vya ugonjwa wa Corona baada ya kufanyiwa vipimo, hali zao zinaendelea vizuri.
“Tumepokea majibu yetu ya vipimo vya Virusi vya ugonjwa wa Corona mimi na Oriana. Na sote Tumekutwa navyo, kwa bahati, tuko katika hali nzuri” alisema Dybala.
Nyota huyo wa Argentina, anakuwa mchezaji wa tatu wa klabu ya Juventus kuwa na maambukizi ya Virusi vya ugonjwa wa Corona baada ya Daniele Rugani pamoja na Blaise Matuidi.
Ikumbukwe kwamba shughuli zote za Michezo nchini Italia zimesimishwa hadi Aprili 30 kutokana na janga hilo la Corona ambalo linaisumbua Dunia kwa sasa.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages