RAIS wa zamani wa klabu ya Real Madrid, Loranzo Sanz amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 76 baada ya kulazwa Hospital kutokana na maambukizi ya Virusi vya ugonjwa wa Corona.
Taarifa za kifo chake zimethibitisha na mtoto wake, Fernando, kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter.
Sanz aliachukua kijiti cha kuiongoza Real Madrid mwaka 1996 kutoka kwa Ramon Mendoza na aliongoza klabu hiyo hadi mwaka 2000.
Katika uongozi wake, Sanz alifanikiwa kusajili wachezaji nyota kama vile, Robert Carlos, Davor Suker, Clareences Seedorf na Predrg Mijatovic.
Ubingwa wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya ulikuwa mwaka 1998 ni baada ya miaka 32 kupitia kwa klabu hiyo bila kutwaa Ubingwa huo wa Ulaya (mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1966) na ubingwa wake wa pili wa Ulaya ulikuwa mwaka 2000.
Mwaka 2000 baada ya Ubingwa wake wa pili wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kama Rais wa Madrid, Sanz alishindwa Uchaguzi na Florentino Perez.

No comments:
Post a Comment