WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR APOKEA VIFAA MBALI MBALI VYA AFYA KUTOKA KWA MFANYA BIASHARA SAID NASSIR NASOR (BOPER) - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, March 31, 2020

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR APOKEA VIFAA MBALI MBALI VYA AFYA KUTOKA KWA MFANYA BIASHARA SAID NASSIR NASOR (BOPER)

Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed (kulia) akikabidhiwa Vifaa mbalimbali na Mfanya Biashara Said Nassir Nasor (BOPER) kusaidia wenye maradhi mbalimbali ikiwa pamoja na Korona miongoni mwa Vifaa hivyo ni Vitanda, Mashuka Sabuni za Kunawa mikono, Viti vya Walemavi na Dawa mbalimbali hapo Wizara ya Afya Zanzibar.
Vifaa mbalimbali vikitolewa na mfanya biashara Said Nassir Nasor (BOPAR) wa kwanza kushoto kwa ajili ya kusaidia wenye maradhi mbalimbali ikiwa pamoja na Korona miongoni mwa Vifaa hivyo ni Vitanda, Mashuka Sabuni za Kunawa mikono, Viti vya Walemavi na Dawa mbalimbali hapo Wizara ya Afya Zanzibar.
Vifaa mbalimbali vikitolewa na mfanya biashara Said Nassir Nasor (BOPAR) kwaajili ya kusaidia wenye maradhi mbalimbali ikiwa pamoja na Korona miongoni mwa Vifaa hivyo ni Vitanda, Mashuka Sabuni za Kunawa mikono, Viti vya Walemavu na Dawa mbalimbali hapo Wizara ya Afya Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Waandishi wa Habari katika Hafla ya kukabidhi Vifaa mbalimbali kusaidia wenye maradhi mbalimbali ikiwa pamoja na Korona miongoni mwa Vifaa hivyo ni Vitanda, Mashuka Sabuni za Kunawa mikono, Viti vya Walemavi na Dawa mbalimbali hapo Wizara ya Afya Zanzibar. (Picha na Yussuf Simai, Zanzibar)

Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar

Wizara ya Afya Zanzibar imepokea msaada wa vifaa mbali mbali vya afya kutoka kwa Mdau wa Maendeleo Said Nassir Nassor Bopar kwa ajili ya kupambana na kujikinga na maambukizi ya Corona.

Akipokea msaada huo Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed huko katika Wizara ya Afya Mnazi mmoja amesema vifaa hivyo vitasaidia kutoa huduma mbali mbali za matibabu pamoja na kupambana na ugonjwa wa corona nchini.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na vitanda 36, mashuka, sanitizer, friji la kuhifadhia damu, mashuka, mask, mito na kiti cha kubebea wagojwa ambavyo vitasaidia kutoa huduma na kujikinga maambukizi ya corona.

Amesema serikali inahitaji vifaa vingi kutokana na kuwepo kwa wagonjwa ambao wanahitaji kupatiwa matibabu na wananchi kujikinga maambukizi ili yasienee nchini.

“Mdau huyu wa maendeleo ameleta vifaa hivi wakati mzuri kwa kuangalia shida iliopo hivi sasa kutokana na kufunguliwa kituo kipya cha kidimni ambacho kinahitaji vifaa mbali mbali kwa wagonjwa waliopata maambukizi ya Corona”, alifahamisha Waziri Hamad.

Aidha Waziri wa Afya amemshukuru Mfanyabiashara huyo kwa msaada huo ambao utasaidia kutoa huduma mbali mbali kwa wagonjwa na kupunguza maambukizi  pamoja kuweza kupambana na kupiga vita ugonjwa wa Corona.

Hata hivyo Waziri huyo amewataka wananchi kuchukua tahadhari za mapema kwa kuepuka mikusanyiko na kufuata maagizo yanayotolewa na serikali ili kujikinga na maambukizi ya Corona.

“Wananchi wasikae vikundi vikundi wabakie Majumbani mwao na kuwadhibiti watoto wao kufanya hivyo kutasaidia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona nchini”, alisema Waziri wa Afya.

Ameitahadharisha jamii kuchukua tahadhari ya kukaa umbali wa mita moja na kufuata maadili na masharti ya wataalamu wa afya kufanya hivyo kutasaidia kuepusha ongezeko la maambukizi kwa kufanya hivyo kutapunguza kusambaa kwa maambukizi hayo.

Alisisitiza kuwa wananchi ambao wana wagonjwa katika hospitali kuu ya Mnazi mmoja kupanga utaratibu wa kuwahudumia wagonjwa wao kuingia  watu wawili tu ili kuepusha msongamano mkubwa ambao utahatarisha maisha yao kwa kupata maambukizi mapya ya Corona.

Nae Mdau wa Maendeleo ambae ni Mfanyabiashara Maarufu Said Nassir Nassor Bopar alisema ametoa msaada huo kwa lengo la kuokoa maisha ya jamii kutokana na hali halisi iliyopo ya mripuko wa maradhi ya corona pamoja  na kujikinga maambukizo hayo.

Alieleza kuwa ataendelea kuisaidia serikali kila hali inaporuhusu ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi pia anatarajia kutoa msaada mwengine  katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A pamoja na Kisiwani Pemba.

“Kila panapotokea tatizo kupenda kuisaidia jamii ili kuepukana na athari ambazo zitaweza kujitokeza tuweze kuzikabili kwa namna moja au nyengine kwa wakati muafaka” alisema Bopa.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages