Bw. Moses Hella, Mkurugenzi wa kampuni ya Emotec Limited,
inayojishughulisha na mifumo mbali mbali ya kiteknolojia ya kibunifu, akielezea
mfumo mpya wa kamera unaoweza mtambua mtu mwenye homa kali kwa muda mfupi, hivi
karibuni jijini Dar es Salaam. Mfumo huo umelenga katika kuisaidia serikali
kwenye janga la Covid19.
Na
Mwandishi Wetu
Kampuni
inayoshughulika na masuala ya teknolojia iliyoanzishwa na Watanzania 'EMOTEC',
imebuni mfumo wenye uwezo wa kumtambua mtu mwenye homa kali, ndani ya muda
mfupi.
Homa kali ni miongoni mwa dalili za mtu aliyeathirika na Ugonjwa wa COVID-19, unaosababishwa na Virusi vya Corona.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa teknolojia hiyo, jijini Dar es
Salaam, Moses Hella, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, amesema mfumo huo unafanya
kazi pindi unapowekwa katika kamera.
Hella
amesema kamera yenye mfumo huo, ina uwezo wa kutambua watu wengi wenye homa
kali, ndani ya muda mfupi. Ambapo hutambua joto la mtu mmoja, ndani ya sekunde
chache.
"Sasa
hivi mtu anawekea kipimo karibu sana kitendo cha hatari. Kutokana na hilo
tumewaletea kamera hizi ambazo zinaweza kutambua joto la mtu, kutoka umbali wa
kutosha. Kamera ionyesha mfano yule mwenye nguo fulani ana joto lisilo la
kawaida.
Inaweza
kumtambua kila mmoja kwa sekunde, na kutambua watu wengi kwa wakati
mmoja," amesema Hella.
Hella
amesema EMOTEC imeamua kuvumbua teknolojia hiyo, ili kuunga juhudi dhidi ya
mapambano ya kudhibiti ueneaji wa virusi hivyo.
"Hizi
camera zinaweza kuwa mbali mita 1.5, wakati vile vifaa vya kupima, mtumishi
huwa karibu zaidi, lazima umsogelee zaidi mhusika. Ni hatari zaidi,"
amesema Hella.
Hella
amesema kamera hizo zinauzwa kulingana na ubora wake, ambapo kima cha chini,
kamera moja inauzwa kuanzia Sh. 1 milioni.
"Zipo
kamera za kushika mkononi zenye uwezo wa kutambua umbali mrefu na za kufunga.
mara nyingi kamera hizi zinatumika maeneo yenye mkusanyiko," amesema
Hella.
Wakati huo
huo, Hella amesema kampuni yake imebuni kamera kwa ajili ya ulinzi wa nyumba,
barabarani na kwenye sehemu za biashara.
Amesema
kamera hizo zina uwezo wa kutoa taarifa pindi linapotokea tatizo katika maeneo
zilipofungwa.
Amesema
mmiliki wa kamera hizo ana uwezo wa kuzungumza na mgeni aliyeko nje, huku yeye
akiwa ndani.
"Kwa
wafanyabaishara, umeajiri watu tunakupa kifaa cha kufungua milango. Ambacho
hakitumii nyilwa 'password'. Kwa kuzingatia changamto hii tumebuni kifaa
kinachofungua kulingana na sura ya mtu. Ambaye imeorodheshwa katika kifaa
hicho.
Pia,
tunawafungia kamera ambazo zina uwezo mkubwa zaidi ya nyumbani. Zina uwezo wa
kutambua kitu fulani kimeingia na kutoka. Zina uwezo wa kutambua kama ni gari
au mtu. Kama ni kiumbe kisicho na athari haiwezi piga kelele," amesema
Hella.
Amesema
mmiliki wa kamera hizo ana uwezo wa kufahamu kila kinachojiri hata akiwa mbali
na nyumbani kwake.
"Kwa
kutumia kamera hii, mtu akiingia kwenye mpaka wako ulioweka kwenye mfumo huo,
inakuanbia mtu kaingia, na unaweza kuamuru kamera ipige kelele na kupelekea mtu
kukimbia.
Chochote
kinachoingia ndani ya eneo lako kamera inapiga kelele," amesema Hella.
Amesema
kamera hizo zimeboreshwa kiasi kwamba zinaonyesha picha vizuri hata wakati wa
usiku.
"Kamera
tumeziboresha kiasi kwamba, usiku unaona clear na ukisafiri mikoani, unaangalia
mubashara 'live' kinachoendelea. Tumeshusha gharama kwa sababu inarekodi pale
ambapo tukio linatokea," ameeleza Hella.
No comments:
Post a Comment