KAMPUNI YA ‘G1 SECURITY’ YAMPATIA RC MAKONDA MCHANGO WA ‘GENERATOR’ KWAAJILI KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA CORONA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, April 3, 2020

KAMPUNI YA ‘G1 SECURITY’ YAMPATIA RC MAKONDA MCHANGO WA ‘GENERATOR’ KWAAJILI KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA CORONA


Kampuni ya Ulinzi ya G1 Ltd leo imeunga mkono Juhudi za serikali ya Mkoa wa Dar es salaam katika Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona kwa kutoa Generator moja kwaajili ya kuzalisha umeme kwenye Vituo vilivyotengwa kwaajili ya tatizo la Corona kama ikitokea dharura ya umeme ukikatika.

Akipokea Mchango huo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda, Mganga mkuu wa Mkoa huo Dr. Rashid Mfaume ameishukuru Kampuni hiyo kwa kuunga mkono juhudi za serikali ambapo ameeleza licha ya kutoa Generator hiyo pia walitoa Ambulance moja ambayo inaendelea kutoa huduma kwenye Hospital ya Mloganzila.

Kwa upande wake Afisa rasilimali watu wa Kampuni ya G1 Security Ltd Bw. Seleman Yusuph amesema Kampuni hiyo itaendelea kushirikiana ofisi ya Mkoa katika masuala mbalimbali ya kijamii.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages