RC MAKONDA ARUHUSU BODABODA NA BAJAJI KUINGIA KATIKATI YA JIJI KIPINDI HIKI CHA JANGA LA CORONA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, April 1, 2020

RC MAKONDA ARUHUSU BODABODA NA BAJAJI KUINGIA KATIKATI YA JIJI KIPINDI HIKI CHA JANGA LA CORONA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo April Mosi ameruhusu Pikipiki na Bajaji kuingia katikati ya Jiji kwaajili ya Kubeba Abiria kwa Sharti la kuhakikisha wanavaa Kofia ngumu (helmet) na kutokuingia katika Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi hadi Ugonjwa wa Corona utakapomalizika.

RC Makonda amefikia uamuzi huo baada ya kushuhudia adha ya Usafiri wanayopata Wananchi kufuatia agizo la Daladala zote kutakiwa kutozidisha abiria (level seat) jambo lililosababisha baadhi ya abiria kuchelewa kazini, kuachwa kwenye vituo na tatizo la msongamano wa watu vituo vya daladala.

Aidha RC Makonda ameielekeza Mamlaka ya Usimamizi wa usafiri wa Ardhini (LATRA) kuhakikisha inakutana na Chama cha Wamiliki wa Daladala ili wafanye mabadiliko ya Route za Daladala kabla ya kesho saa sita mchana baada ya kubaini kuwepo kwa baadhi ya Wamiliki wa Daladala walioamua kusitisha kutoa huduma za usafiri kutokana agizo la serikali kutaka Daladala zisijaze abiria.

Hata hivyo RC Makonda amewaomba wananchi kuendelea kuchukuwa tahadhari dhidi ya Corona kwa kuhakikisha wanazingatia maelekezo yote yanayotolewa na Wizara ya Afya.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages