RC MAKONDA asema WATAKAOKAMATWA kwa UZURURAJI watapewa ADHABU za kusafisha MITARO - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, April 6, 2020

RC MAKONDA asema WATAKAOKAMATWA kwa UZURURAJI watapewa ADHABU za kusafisha MITARO


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema zoezi la kuwakamata wazururaji katika mkoa huo limeanza rasmi leo ambapo wazururaji watakaokamatwa watapewa adhabu mbalimbali ikiwemo Kusafisha mitaro, Kusafisha barabara, kufyeka nyasi na kulima bustani.

RC Makonda amesema kama kuna watu walidhani watapelekwa mahabusu na kula Chakula cha bure wasahau kabisa jambo hilo.


Mhe. Makonda ametoa kauli hiyo wakati wa Uzinduzi wa Shoppers Supermarket ya Mlimani City ambapo ameonyesha kufurahishwa na uwekezaji uliofanyika na wazawa jambo lililosaidia zaidi ya Vijana 205 kupata Ajira kwa Shoppers ya Mliman City pekee.

Aidha RC Makonda amesema uwepo wa Supermarket hiyo licha ya kuwezesha wananchi kupata mahitaji muhimu pia serikali inapata Kodi ambapo inaelezwa kwa kipindi cha miezi nane pekee ambayo Jengo hilo kikifungwa serikali ilikosa kodi ya shilingi Bilioni 28.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema uwepo wa Supermarket hiyo pia utawezesha Wafugaji na Wakulima wa Mazao ya Matunda na Mbogamboga kupata sehemu ya kuuza Mazao yao.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages