WAGONJWA WAPYA 14 WA CORONA WAONGEZEKA TANZANIA, SASA WAFIKIA 46 - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, April 13, 2020

WAGONJWA WAPYA 14 WA CORONA WAONGEZEKA TANZANIA, SASA WAFIKIA 46


Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa taarifa ya ongezeko Ia wagonjwa kumi na nne (14) wa Corona (COVID-19) nchini hadi kufikia 46 kutoka 32 tuliowatolewa taarifa ya awali tarehe 10 Aprili, 2020. 

Katika taarifa hiyo imesema kuna Wagonja wapya 14 wote ni Watanzania. Kati ya hawa Wagonjwa walioko Dar es Salaam ni 13 na mmoja yuko Arusha. 

Wagonjwa wote wanaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa wataalam wa afya. Ufuatiliaji wa watu waliokuwa karibu na wagonjwa unaendelea. 

Kwa mara nyingine Serikali inarudia tena kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huu kama tunavyowapatia taarifa na elimu mara kwa mara kupitia njia mbali mbali na hususan kuepuka misongamano na mikusanyiko isiyokuwa ya lazima.


No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages