Watu
wawili wamefariki Dunia kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha kwa siku tatu
mfululizo katika wilaya ya Arumeru
Akitoa
Taarifa za hali ya mwendendo wa mvua hizo mara baada ya kufanya ziara na
kushiriki shughuli za uokoaji, Mkuu wa wilaya ya Arumeru amesema mvua zimeleta
madhara makubwa kufuatia watu wawili kufariki leo Alhamisi Tarehe 23/04/2020
Katika Halmashauri ya Meru
DC
Muro amewataja waliokufa kuwa ni Ndugu Kifo Terevaeli mirisho nasari Mwenye
miaka 65 Mkazi wa kitongoji cha meto kijiji cha mulala kata ya songoro, ambapo
amefariki Dunia Asubuhi baada ya maporomoko ya Udongo kutoka mlimani kuvunja
ukuta wa chumba alichokuwa amelala na kufariki Dunia papo hapo, na tayari mwili
wake umepatikana na kupelekwa katika hospital ya Mount Meru.
DC
Muro pia amesema kifo kingine na ni cha mtoto alietambuliwa kwa majina ya Tumaini Simon Mwenye umri wa miaka 3 Mwenyeji
wa kijiji cha Valeska Kitongoji cha Mwamko, ambae amesombwa na mafuriko ya maji
wakati akiwa katika harakati za kuokolewa na Mzazi wake ambapo Mzee simon
alifanikiwa kuokoa mtoto mmoja na mwingine kufariki dunia na mwili wa mtoto
tumaini umepatikana na taratibu za mazishi zinaendelea.
Katika
Mvua hizo DC Muro amesema zaidi ya Nyumba 50 zimeharibiwa uku zingine
zikianguka kutokana na maji kuwa mengi na tayari ameshaziagiza kamati za maafa
zinazonongozwa na wakurugenzi wa Halmashauri za Meru na Arusha kushirikiana na
wananchi katika kutoa misaada ya haraka katika kunusuru familia hizo ikiwemo
kuwatafuta makazinya muda, na kutoa tahadhari ya wananchi waliojenga pembeni ya
milima na miinuko mikubwa pamoja na wale waliojenga Katika maeneo yanayokumbwa
na mafurko kuondoka katika maeneo yao haraka kabla ya madhara zaidi mana mvua
bado zinaendelea kunyesha.


No comments:
Post a Comment