JECHA SALUM JECHA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, June 20, 2020

JECHA SALUM JECHA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR




Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar Jecha Salum Jecha leo Juni 20 amejitokeza mbele ya Ofisi ya Chama cha Mapinduzi CCM kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea kiti cha Urais wa Zanzibar katika uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba kupitia Chama Cha Mapinduzi.

Jecha amechukua fomu hiyo leo Jumamosi Juni 20, 2020 kwenye ofisi za CCM zilizopo Kisiwandui Zanzibar.

Jecha anakuwa mwanachama wa kumi na nne (14) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Credit – Malunde 1 blog

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages