MCHIMBAJI MDOGO WA MADINI YA TANZANITE KUTAMBULIWA RASMI KUWA BILIONEA BAADA YA KUPATA MAWE MAWILI YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 7.8 - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, June 24, 2020

MCHIMBAJI MDOGO WA MADINI YA TANZANITE KUTAMBULIWA RASMI KUWA BILIONEA BAADA YA KUPATA MAWE MAWILI YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 7.8

Mawe makubwa mawili ya Tanzanite moja lina kilo 9.2 ambalo lina thamani ya shilingi bilioni 4.5 na la pili lina kilo 5.8 lenye thamani shilingi bilioni 3.3.
Afisa Madini akionyesha moja ya jiwe la Tanzanite lilipatikana
 
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila amesema kuwa leo Wizara inamtabua Mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite Bw. Saninniu Laizer kuwa bilionea baada ya kupata  mawe  makubwa mawili yenye thamani ya shilingi  bilioni 7.8.

Katibu Mkuu amesema kuwa mchimbaji huyo amepata mawe hayo mawili ambapo moja lina kilo 9.2 ambalo lina thamani ya shilingi bilioni 4.5 na la pili lina kilo 5.8 lenye thamani shilingi bilioni 3.3.

Mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite Bw. Saniniu Laizer  bilionea mpya Tanzania
 
“Na utofauti wake ni kwamba mawe ya uzito huo hayajawahi kupatikana kwenye machimbo ya tanzanite tangu machimbo yaanze na yamepatikana ndani ya ukuta wa Mirereni kwahiyo hii ni rekodi mpya ya kupata mawe yenye uzito huo” amesema Prof. Msanjila
 
Profesa Msanjila amesema kuwa sekta ya madini inauwezo wa kumfanya mtu kuwa bilionea kwa haraka, ameongeza kuwa kunahitaji kuwa uwekezaji wa dhati katika sekta hiyo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages