WANAWAKE WAJASIRIAMALI VISIWANI PEMBA WASHAURIWA KUTUMIA VIZURI NEEMA YA ZAO LA KARAFUU ILI KUZALISHA BIDHAA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, June 27, 2020

WANAWAKE WAJASIRIAMALI VISIWANI PEMBA WASHAURIWA KUTUMIA VIZURI NEEMA YA ZAO LA KARAFUU ILI KUZALISHA BIDHAA

 
Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA-Zanzibar Dkt,Mzuri Issa (katika) akitazama baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wajasriamali kisiwani Pemba,kulia ni Asha Mussa Afisa uwezeshaji uchumi TAMWA ofisi ya Pemba kushoto ni Sakina Bakari Ame.

Na Muhammed Khamis-TAMWA-Zanzibar
MKURUGENZI  wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake( TAMWA- Zanzibar)  Dkt.Mzuri Issa amewashauri wanawake wajasiriamali kisiwani Pemba kutumia  vizuri neema ya zao la Karafuu kisiwani humo kwa  kuzalisha bidhaa mbali mbali.

Dkt Mzuri aliyasema hayo leo Juni 27,2020 wakati alipokua akitizama baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wajasirimaali hao kutoka Pemba huko ofisini kwake Tunguu Wilaya ya kati Unguja.

Amesema zao la karafuu linaweza kuzalisha bidhaa mbali mbali ambazo zinasoko kubwa ndani na je ya Nchi iwapo wajasiriamali hao wataweza kuzisanifu vyema karafuu hizo.

Akitolea mfano wa bidhaa zinazotokana na karafuu alisema ni sabuni pamoja na liwa ambalo ni maalumu na hutumika kwa ajili ya kusafishia mwili kwa wanawake na wanaume (singo)

Pia Dkt, Mzuri aliwataka wajasiriamali hao kuanza kuangaza zaidi soko la kimataifa ambapo pia kuna uhitaji mkubwa wa bidhaa za asili kutoka Zanzibar hususani zinazoalishwa kwa kutumia karafuu na mengineyo.

Kwa upande wake afisa uwezeshaji wanawake TAMWA ofisi ya Pemba Asha Mussa alisema wanawake wengi kisiwa cha Pemba wamehamasika na kujiunga  kwenye vikundi mbali mbali vya uzalishaji wa bidhaa.

Akitolea mfano alisema pia wajasiriamali hao hawakuridhika tu na uzalishaji wa bidhaa hizo pia wameanza kujiungiza katika ufuagaji ambapo tayari baadhi ya vikundi vinamiliki mabanda ya na wanaendelea na ufugaji kuku.

Akizungumzia kuhusu changamoto alisema bado zipo changamoto mbali mbali  ikiwemo ukosefu wa soko la uhakika kwa wajasiriamali ambapo wakati mwengine wajasirimali hao hulazimika kukaa na bidhaa zao ndani kwa muda  mrefu.

Afisa huyo uwezeshaji wanawake kiunchumi aliomba Serikali na taasisi nyengine mbali ndani ya Zanzibar na nje ya Tanzania kujitokeza kwa wingi kuunga mkono jitihada za vikundi hivyo kwa kuwa kufanya hivyo kutawawezesha wanawake wengi kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini.

Akizungumzia kuhusu hali halisi ya uzalishaji wa bidhaa mmoja miongoni mwa wajasiriamali kutoka kisiwani Pemba Sakina Ame Bakar alisema wanajitahidi katika uzalishaji wa bidhaa  bora na zenye viwango vya hali ya juu.

Alisema licha ya jitihada hizo lakini wanaendelea kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa soko bora na lenye uhakika kwao ambalo lingewafanya kwa wajasiriamali bora na wakimataifa.

Aidha ameiomba Serikali kuendelea kuwatengezea mazingira ikiwemo kuwakutanisha na makampuni makubwa pamoja na wajasiamali wengine wa  kimataifa ili waweze kutengeza masoko mapya.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages