Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo akipokea msaada mabati 180 kutoka kwa
Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Seka Urio.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Turiani
wakipeleka madawati darasani baada ya hafla fupi ya makabidhiano na Benki ya
NMB.
Benki ya NMB, imekabidhi
misaada ya mabati 180, madawati 200, mashine sita za kunawia mikono, viti na
meza 100, kwa ajili ya Shule za Msingi Oysterbay, Msasani, Tandale Magharibi,
Mzimuni na Kisauke pamoja na Sekondari ya Turiani. Huku kituo cha Afya cha Mabwepande
kikipata vitanda magodoro, vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya jumla ya Sh.
Mil. 36.
Akizungumza wakati wa hafla
ya kuvibabidhi kwa Mkuu wa Wilaya, Daniel Chongolo, Kaimu Meneja wa Benk ya NMB
Kanda ya Dar es Salaam, Seka Urio alisema “Ingawa Serikali inafanya
makubwa, sisi kama wadau tunawajibu wa kuunga mkono juhudi hizi za maendeleo
kwa kusaidia jamii, kwani kupitia jamii hii hii, ndio imeifanya benki yetu kuwa
hapa ilipo, kubwa kuliko benki yoyote hapa nchini huku tukiendelea kupokea tuzo
ya benki bora kwa mara ya nane mfululizo,”
Alibainisha kuwa, NMB
itaendelea kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo katika jamii
inayowanzunguka. “Kwa maana hiyo, NMB tumeamua kushirikiana na shule hizo,
ambazo kila shule inapata madawati 50 na viti vyake. Pia tumechangia Shule ya
Msingi Mzimuni mabati 150, huku Shule tano zikipata mashine za kunawia mikono
na maji tiririka ilikuzuia maambukizi ya Covid-19,” aliongeza:
Kwa mwaka 2020, NMB imetenga
zaidi ya Sh. Bilioni 1 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii ikiwemo
kusaidia sekta ya afya na elimu, kiasi kinachoifanya kuwa benki ya kwanza
katika kuchangia maendeleo kuliko benki yoyote nchini.
Kwa upande wake, DC Chongolo
aliipongeza Benki ya NMB kwa moyo wa kuijali na kuithamini jamii na kwamba
misaada mbalimbali inayotoa katika sekta za afya na elimu, inaacha alama njema
katika mioyo ya wanafunzi, walimu na jamii kwa ujumla na kuwa inasaidia
harakati za Serikali katika kuboresha miundombinu na kutatua changamoto.
Chongolo aliwaagiza
watendaji mbalimbali waliopo katika Wilaya ya Kinondoni, kuhakikisha wanatumia
huduma za NMB hasa za makusanyo ya kodi, ili kuchagiza pato la benki hiyo na
kukuza asilimia moja ya mapato yao yamwaka na kuzifikia taasisi nyingi zaidi
zenye uhitaji kupitia program ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).
No comments:
Post a Comment