RC MAKONDA AWAAGIZA TAKUKURU KUFANYA UCHUNGUZI WA BILION 33 ZA MIKOPO YA 10% ZA MANISPAA KAMA INAWAFIKIA WALENGWA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, July 1, 2020

RC MAKONDA AWAAGIZA TAKUKURU KUFANYA UCHUNGUZI WA BILION 33 ZA MIKOPO YA 10% ZA MANISPAA KAMA INAWAFIKIA WALENGWA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewataka Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
TAKUKURU kuanza Mara moja uchunguzi Fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 33 za mikopo ya 10% iliyotengwa kwaajili ya makundi ya Vijana, Kinamama na Walemavu katika Halmashauri kama fedha hizo zinawafikia kwa walengwa.

RC Makonda ametoa agizo hilo wakati wa Mwendelezo wa Ziara ya Kukabidhi Miradi kwa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Ubungo na kuwaelekeza kuhakikisha kabla ya Julai 20  anapatiwa mchanganua wa namna pesa hiyo imetumika kwakuwa Rais Magufuli aliondoa Riba kwenye mkopo huo ili kuyawezesha kiuchumi makundi hayo.

Katika ziara hiyo RC Makonda amekabidhi miradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 559.6 kwa Chama cha Mapinduzi kwa upande wa Jimbo la Ubungo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho.

Miongoni mwa Miradi aliyokabidhi ni Daraja la Juu Ubungo lenye thamani ya Bilioni 299, Upanuzi wa Mto Ng'ombe Bilioni 32.5, Ujenzi wa Barabara ya Shekilango na Viunga vyake Bilioni 26 na Ujenzi Wa jengo la Wodi ya Wagonjwa na Upasuaji Hospital ya Palestina.

Miradi mingine aliyokabidhi RC Makonda ni Ujenzi miundombinu ya Madarasa 8, Matundu 12 ya Vyoo na uzio kwenye Shule ya Ubungo plaza pamoja na kukagua Vikundi 20 vya wajasiriamali waliokopeshwa fedha kupitia 10% za Manispaa.

Ziara hiyo itaendelea tena siku ya kesho kwa majimbo ya Ilala, Segerea na Ukonga ambapo atakabidhi miradi mbalimbali ya Maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages