Dar es Salaam. RAIS Dk.John Magufuli amtengaza rasmi kwamba kuanzia sasa Uwanja wa Taifa utajulikana kwa jina la Uwanja wa Mkapa kama hatua ya kuenzi na kumkumbuka Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa katika sekta ya michezo.
Dk.Magufuli ametangaza uamuzi huo leo Julai 28, 2020 alipokuwa akihutubia taifa juu ya maisha ya Rais Mstaafu Mkapa katika uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam wakati wa shughuli ya kitaifa ya kumuaga Rais Mstaafu Benjamini Mkapa aliyefariki dunia usiku wa Julai 23-2020.
Amesema baada ya kifo cha mzee Mkapa kumekuwepo na maombi mbalimbali ya wadau wa michezo na Watanzania wanaotaka uwanja wa mpira wa Taifa upewe jina la Mkapa, hivyo amekubaliana na maombi hayo.
"Mzee Mkapa alisimamia vema suala la michezo, sanaa na burudani."
Uwanja wa mpira wa miguu unaofahamika Uwanja wa Taifa ni matokeo ya jitihada hizo, hata hivyo mzee Mkapa hakupenda sana vitu viitwe kwa jina lake. na kwa kuwa leo amelala usingizi najua hawezi kumuadhibu.
"Hivyo uwanja huu kuanzia sasa utaitwa Uwanja wa Mkapa au Mkapa Stadium kama sehemu ya kumuenzi kwa jitihada zake katika michezo. Mzee Mkapa alikuwa mwanamichezo mzuri na alikuwa shabiki wa Yanga."
"Ingawa hakuwahi kuniambia ingawa hata Rais mstaafu mzee Jakaya Kikwete amethibitisha hilo kwa kuwa na yeye ni Yanga, sijajua tu mzee Mwinyi yeye ni shabiki wa timu gani." Amesema Rais Magufuli.
Ameongeza kwamba hata COSOTA ambayo inahusika na haki za wasanii katika kunufaika na kazi zao ilianzishwa na mzee Mkapa.
Ameongeza kwamba hata COSOTA ambayo inahusika na haki za wasanii katika kunufaika na kazi zao ilianzishwa na mzee Mkapa.
No comments:
Post a Comment