BENKI YA NBC YAJIDHATITI KUSAIDIA SEKTA YA MADINI KWA WACHIMBAJI WADOGO - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, September 17, 2020

BENKI YA NBC YAJIDHATITI KUSAIDIA SEKTA YA MADINI KWA WACHIMBAJI WADOGO

 
 
Meneja Huduma na Bidhaa wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Makao Makuu, Jonathan Bitabajaji akitoa mada wakati wa semina maalumu ya wachimbaji wadogo na wadau wa madini ya Dhahabu yaliyodhaminiwa na Benki hiyo katika maonyesho ya madini yanayofanyika Mjini Geita.
 
Washiriki mbalimbali ambao ni wadau na wachimbaji wadogo wanaoshiriki semina maalum ya mafunzo ya siku tatu yaliyoandaliwa na kudhaminiwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakati wa Maonesho ya tatu ya Sekta ya Madini ya Dhahabu yanayofanyika katika Viwanja vya Bombambili Geita.
 
Maofisa wa Benki ya Taifa Ya Biashara (NBC) Mariam Benjamini (mwenye Fulana Ya Bluu) na Modester Johanson (wa kwanza kulia) wakifuatilia kwa ukaribu Mada iliyokuwa ikitolewa na Meneja Huduma na Bidhaa wa Benki hiyo kutoka Makao Makuu Jonathan Bitabajaj.
 
Meneja Huduma na Bidhaa wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Makao Makuu Jonathan Bitabajaji (katikati) akizungumza jambo na Meneja Masoko wa Benki hiyo Alina Kimanyo (wa kwanza kushoto) na Ofisa Masoko kwa wateja wadogo na wakati Esther Kahabi (wa kwanza kulia) katika Banda lao la Maonesho ya Sekta ya Madini yaliyodhaminiwa na Benki hiyo. 
 
Meneja Mahusiano kwa wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Mkoa wa Mwanza Mariam Benjamin (aliyesimama) akizungumza jambo na mmoja wa Mawakala wa Benki hiyo aliyepo ndani ya Banda la NBC kwaajili ya kutoa huduma za Kifedha kwa wateja wa Benki hiyo.
 

 
Meneja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Tawi la Geita, Hilda Bwimba (aliyesimama) akizungumza na Ofisa wa Benki hiyo kutoka Makao Makuu Dar es Salaam Modester Johanson (aliyekaa chini) katika maonyesho ya Madini yanayoendelea Mjini Geita.
 
Ofisa wa Benki ya NBC kutoka Makao Makuu Dar es Salaam, Modester Johanson (aliyekaa chini) akifafanua jambo kwa Meneja wa Benki hiyo tawi la Geita, Hilda Bwimba (kulia aliyesimama) na Meneja uhusiano kwa wateja Binafsi Mkoa wa Mwanza, Mariam Benjamini (kushoto mwenye fulana ya Bluu) katika maonyesho ya Madini yanayoendelea Mjini Geita.
 
Meneja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Tawi la Geita Hilda Bwimba (wakwanza kulia) akielekeza jambo kwa watumishi wenzake wa Benki hiyo walipokuwa kwenye Banda lao katika Maonyesho ya Sekta ya Madini yanayofanyika kwa siku 11 katika viwanja vya Bombambili Mkoani Geita. (wakwanza kushoto ni Mariam Benjamini Meneja Mahusiano kwa wateja Binafsi Mkoa wa Mwanza na (katikati) ni Ofisa wa Benki hiyo kutoka Makao Makuu Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages