
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Makampuni na Majina ya Biashara wa Wakala wa usajili wa Makampuni (BRELA) Mainrad Rweyemamu (kulia) akizungumza na mgeni aliyefika kwenye banda la Taasisi hiyo kupata taarifa mbalimbali za Taasisi hiyo kwenye maonyesho ya tatu ya sekta ya viwanda yanayoendelea Mjini Geita.
Ofisa Habari Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA) Christina Njovu (kulia) akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu Taasisi hiyo alipofika kwenye banda lao kwaajili ya kupata habari na taarifa mbalimbali za Taasisi hiyo.
Msaidizi wa Usajili wa Wakala wa usajili wa Makampuni (BRELA) Walter Masamu (mwenye fulana nyeusi) akizungumza na wananchi waliofika kwenye Banda la Taasisi hiyo kwenye maonyesho ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya Bombambili Mjini Geita.
Msaidizi wa usajili Mkuu wa Wakala wa usajili wa Leseni (BRELA) Hellen Mhina akimkabidhi moja ya mwananchi aliyefika kwenye Banda la 'Clinic' ya Biashara kupata maelezo mbalimbali yanayohusu Taasisi hiyo.

Mtaalam wa mifumo ya Kompyuta Kutoka BRELA Hillary Mwenda akitoa Elimu ya ujasiliamali wakampuni kwa mjasiliamali anayeshiriki maonyesho ya Madini Mjini Geita.

Afisa kutoka kwenye Taasisi hiyo Athumani Makuka BRELA Hillary Mwenda akitoa Elimu ya Usajiri wa Kampuni ya usajiri wa Makampuni kwa Mjasiliamali aliyepo katika maonyesho ya Madini Mjini Geita.
Na: Richard rusha – GEITA.
KAIMU mkurugenzi wa Idara ya Makampuni na Majina ya biashara Brela Mainrad Rweyemamu amewataka wananchi kuacha kutumia vishoka pindi wanapofanya usajili wa Makampuni kwani kufanya hivyo nikujichelewesha usajili.
Amesema kuwa wao Kama Brela wanakutana na changamoto wakati wakufanya sajili kutokana na mtu anayesajili kampuni wakati mwingine anakuwa si muhusika na hulazimika kumtaka muhusika Jambo ambalo wakati mwingine linamchelewesha kupata usajili wake wa Kampuni au Alama ya jina la kampuni yake.
Rweyemamu ameyasema hayo leo mkoani Geita mbele ya waandishi wa Habari kwenye maonyesho ya kimataifa ya teknolojia ya uwekezaji wa madini ambayo yanaendelea.
"Tunawashauri wadau kuacha kutumia vishoka kwani wakati mwingine watu Hawa wakati wanaweka vizingiti kwa kuchelewesha mtu sahihi kupata usajili wake kutokana tunapohitaki nyaraka kwa wakati panajitokeza changamoto " amesema Rweyemamu.
Amesema kuwa nahata kwenye mawasiliano wao kama Brela watawasiliana na mtu wakati kwasababu yeye ndio anakuwa amekamata usukani Jambo ambalo hawakubaliani nalo na badala yake wanamtaka muhusika mwenyewe ili wawe kuwasiliana moja kwa moja kwa maana mwenye kampuni.
Pia mkurugenzi Rweyemamu amewataka wananchi hususani wafanyabiashara wote hususani Kanda ya ziwa kujitokeza kwenye viwanja vya maonyesho ya madini mkoani Geita ili kupata fursa ya kusajili kampuni yake au majina ya kampuni.
Amesema kuwa wao watakuwa mkoani humo hadi semptemba 27 kwa ajili kuhakikisha wanawapatia huduma wananchi na hivyo wahakikishe wanajitokeza kwa wingi.
Amefafanua kuwa majukumu yao makubwa wao kama brela nipamoja na kufanya usajili wa Makampuni ,uandikishaji wa majina ya biashara ,usajili wa alama za biashara na huduma na kutoa leseni za viwanda vikubwa Daraja pamoja na kusajili Ataza kwa maana ubunifu.
Pia amesema kuwa hivi Sasa kila kitu kinafanyika kwa mtandao hivyo hakuna haja ya kubeba manyaraka mkononi kwa kila kitu kinamalizwa kwa mtanda tofauti na ilivyokuwa awali.
Hata hivyo amesema pamoja na kufanya mambo hayo yote wanatoa na ushauri na kazi yao kubwa nikuwezesha watu kufanya biashara na si vinginevyo.
No comments:
Post a Comment