NATE VISION yaleta FURSA kwa wachimbaji wadogo GEITA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, September 22, 2020

NATE VISION yaleta FURSA kwa wachimbaji wadogo GEITA


GEITA | Richard Mrusha | KAMPUNI ya Nate Vision imewaalika wachimbaji wa madini  ambao wangependa kufanyiwa tafiti katika maeneo yao ya uchimbaji wa madini hususani katika mkoa wa Geita.

Wito huo umetolewa mkoani Geita leo na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Judith Jeremia wakati akizungumza na waandishi wa habari Mara tu baada ya waziri Dotto Biteko kutembelea kwenye banda lake lililopo kwenye viwanja vya Maonyesho Bombambili mkoani humo.

Kwaza amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kutembelewa na Waziri Biteko kwenye banda lake kwani hilo ni Jambo kubwa na lenye furaha katika maisha yake.

Judith amesema kuwa moja ya kazi ambayo anafanya kupitia kampuni yake ni uwezeshaji kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo na kimsingi kampuni yake iliaza na huduma za kuprit mafurana na Mambo mengine lakini kadri walivyoendelea kukua wakaona wajikite kwenye kuwezesha wachimbaji Madini.

"Kupitia elimu niliyoipata ya mazingira licha ya Mambo mengine nimeona kuangalia kwenye sekta ya Madini kwani kuna wachimbaji Wana leseni lakini wnaachimba kwa kubahatisha katika eneo husika kwa kuzingatia hilo wameshirikiana na sido pamoja na wadau wengine kuyaangalia makundi ya akinamama na vijana ili kuwasaidia kuwapa elimu” amesema.

Nakuongeza kuwa "Unajua wadau wengi wanaogopa kufanya tafiti kwa kuhofia gharama hivyo wanawakaribisha wananchi kwenye kampuni yetu kwa lengo la kukubaliana na kufanyiwa tafiti na sisi Kama kampuni hatufanyi tu biashara bali wanafanya na maombi ili shughuli zifanyike kwa kibari Cha Mungu." amesema Judith.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages