Rais Magufuli Alaani Kufuatia Mauaji Ya Kada Wa CCM Njombe Na Iringa - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, September 28, 2020

Rais Magufuli Alaani Kufuatia Mauaji Ya Kada Wa CCM Njombe Na Iringa

Na Amiri Kilagalila | Njombe | Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea wa kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.John Pombe Magufuli, ametuma salamu za pole pamoja na ubani wa shilingi milioni tano kwa familia ya Mlelwa, kufuatia mauaji na kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu (UVCCM) mkoa wa Iringa Ndugu,Emmanuel Mlelwa.


Akitoa salamu za pole katika mazishi yaliyofanyika kijiji cha Luvuyo kata ya Madope wilayani Ludewa, mkoani Njombe, katibu wa NEC Uchumi na fedha wa Chama hicho ambaye pia ni mlezi wa CCM mkoa wa Njombe Dkt.Frank Hawasi. Amesema Rais Magufuli amesikitishwa na kifo cha kijana huyo kutokana na umuhimu wake kwa familia na taifa. 

Mwenyekiti wetu amepokea taarifa ya kifo cha kijana wetu Emmanuel Mlelwa kwa masikitiko makubwa sana,kwasababu sio kifo cha kawaida,lakini pia umuhimu wa kijana mwenyewe kwa nchi kwa ujumla” Alisema Dkt.Hawasi 

Amesema Rais Magufuli amelaani kitendo hicho kwani hakikubaliki katika jamii “mwenyekiti wa CCM Taifa analaani kitendo kilichofanyika kwa ndugu yetu Emmanuel Mlelwa kwasababu hakionyeshi utu, hakionyesho uzalendo na hakionyeshi utanzania wetu” aliongeza Dkt. Frank Hawasi.

Aidha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa kupitia kwa katibu wa NEC Uchumi na Fedha wa Chama hicho taifa Dkt.Frank Hawasi. Ameagiza vyombo vya Dola mkoani Njombe kuwatafuta na kuwabaini waliohusika na mauaji ya kijana huyo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages