WADAU WA SEKTA MADINI WATEMBELEA MGODI WA GGML GEITA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, September 26, 2020

WADAU WA SEKTA MADINI WATEMBELEA MGODI WA GGML GEITA

 

Meneja Mahusiano wa GGML Joseph Mangilima akitoa mada mbele ya wadau mbalimbali waliopo kwenye maonesho ya Sekta ya Madini yanayoendelea Mkoani Geita walipotembelea Mgodi huo kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na GGML.

 
Wadau mbalimbali kutoka kwenye Taassisi za Serikali na Sekta Binafsi, Wajasiriamali na Wafanyabiashara wakiwa kwenye chumba maalumu cha mikutano ndani ya mgodi wa GGML walipofika kujifunza na kujionea Shughuli zinazofanywa na Mgodi huo kwenye Sekta ya uchimbaji wa Madini ya Dhahabu Mkoani Geita.   
 
Meneja Huduma na Bidhaa wa Benki ya (NBC) Makao Makuu Jonathan Bitabajaje (mwenye fulana nyekundu) akiuliza swali mara baada ya kumalizika kwa mada maalum juu ya shughuli za Mgodi huo iliyotolewa na Meneja Mahusiano wa GGML Joseph Mangilima. 

 
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye Bwawa maalumu la kukusanya maji taka kutoka kwenye maeneo yote ya mgodi wa GGML.

Wadau kutoka kwenye Taassisi za Serikali na Sekta Binafsi, Wajasiriamali na Wafanyabiashara wakiwasili kwenye eneo la uchimbaji ndani ya Mgodi huo. 
 
Muonekano wa shimo lenye urefu wa zaidi ya mita 450 ambalo lilikuwa likitumika na kampuni ya GGML kuchimba madini ya Dhahabu.  

 Tito mselem na Godwin Masabala | GEITA | Wadau wa mbalimbali wa Sekta ya Madini walioshiriki Maonesho ya Tatu ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea mkoani Geita Septemba 25, 2020 wametembelea Mgodi wa Geita Gold Mining Limited (GGML) ili kujifunza na kujionea Teknolojia katika Sekta hiyo.

Katika ziara hiyo wadau wote walipatiwa semina elekezi ili kujua Sheria na Taratibu zilizopo katika mgodi huo hususan katika eneo la usalama.

"Sheria inatutaka kama kuna watu wanaokuja kututembelea lazima tuwape semina elekezi katika upande wa Usalama  lakini kwa Wafanyakazi inakuwa ni mafunzo ya muda mrefu, sisi kwetu usalama ndiyo kipaumbele chetu ili kila moja atoke akiwa salama", alisema Afisa Mafunzo Mwandamizi wa GGML. Sebastian Malunde.

Eneo la GGML asilimia kubwa lipo ndani ya msitu wa hifadhi, hivyo mgodi unahakikisha wanyama wanaoishi katika msitu huo wanakuwa salama na pia tunaheshimu utu wa kila moja na kujali mchanganyiko na sio kabila Wala rangi ", aliongeza Malunde.

GGML ambayo ina makao makuu ya Afrika Kusini ndiyo Kampuni ya 3 Duniani inayozalisha Madini ya Dhahabu.

Imeelezwa kuwa, Madini ya Dhahabu yaligunduliwa Geita mwaka 1856 lakini utafiti ulianza mwaka 1936 wakazalisha mpaka 1966 baada ya hapo mgodi ukafungwa mpaka mwaka 1994 ambapo utafiti ukaanza kwa Mara nyingine na Kampuni ya Sammax ili kujilizisha ambapo mwaka 1999 utafiti ukawa umekamilika.

Inasemakana kuwa, Mwaka 2000 uzalishaji ulianza katika mgodi GGML ambapo mpaka sasa mgodi huo unaongoza kwa uzalishaji wa dhahabu Afrika mashariki kuanzia mwaka 2000 hadi 2017 Wakia Milioni 8.3 za dhahabu zilizalishwa.

"Tunajivunia kuwa wachangiaji wakubwa wa maendeleo nchini Tanzania ambapo pia mgodi huo una wafanyakazi zaidi 3500", alisema Meneja Mahusiano Joseph Mangilima.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages