WAZIRI BITEKO AITAKA BRELA KUENDELEZA MAPAMBANO DHIDI YA VISHOKA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, September 21, 2020

WAZIRI BITEKO AITAKA BRELA KUENDELEZA MAPAMBANO DHIDI YA VISHOKA

 
Waziri wa Madini Mh. Dotto Biteko (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Idara ya Makampuni (BRELA) Mainrad Rweyemamu (kulia Mwenye suti) mara baada ya kutembelea Banda la Taasisi hiyo Katika Maonyesho ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya Bombambili Mjini Geita.

 
Waziri wa Madini Mh. Doto Biteko akikabidhi cheti cha usajiri wa jina la biashara kwa Bi Mariam Mollel  cheti ambacho amekipata mara baada ya kusajiri katika banda la BRELA lililopo katika viwanja vya bombambili kwenye maonesho ya tatu ya Teknolojia na uwekezaji sekta ya madini 2020.  
 
Waziri wa Madini Mh. Dotto Biteko (kushoto mwenye fulana nyeusi) akiangalia Cheti cha Usajili wa jina la Biashara kinachotolewa papo hapo kwenye viwanja vya maonyesho ya Madini kabla ya kumkabidhi mjasiliamali aliyefika viwanjani hapo kwaajiliya kupatiwa huduma hili kutoka BRELA.(wakwanza kulia) ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Makampuni (BRELA) Mainrad Rweyemamu.

Waziri wa Madini Mh. Doto Biteko (aliyekaa chini) akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Banda la Wakala wa usajili wa Makampuni (BRELA) katika banda la BRELA lililopo katika viwanja vya bombambili kwenye maonesho ya tatu ya Teknolojia na uwekezaji sekta ya madini 2020.

GEITA | Richard Mrusha | WAZIRI wa Madini Dotto Biteko amewaagiza Wakala wa usajili wa Makampuni na Biashara BRELA kuhakikisha wanapambana kikamilifu watu wanaotumika jumbe kwa njia mitandao kwa lengo la kupotosha umma kwa kujifanya wao ni BRELA wakati sio.

Biteko ameyasema hayo Leo mkoani Geita wakati alipokuwa anatembelea mabanda kwenye maonyesho ya sekta ya Madini yanayoendelea mkoani humo na kupata fursa ya kufika kwenye banda lao ambapo amesema lazima brela wapambane na watu hao.

"Kuna watu bandia ambao wanasumbua wananachi na wengine kuwaibia kwa kujifanya wao ni wafanyakazi wa Brela wakati ni wezi hivyo nivema nyie mkaweka utaratibu mzuri wa kupambna na kundi hili ambalo linatumia jumbe fupi za kwenye mtandao na kuwarubini watu Kama Wao wanafanya usajili."amesema Biteko

Kwaupande wake Kaimu mkurugenzi wa Idara ya Makampuni na Majina ya biashara Brela Mainrad Rweyemamu amesema wao Kama taasisi wamepokea maagizo ya waziri na watayafanyia kazi na kwamba hata hivyo wameshaaza kuchukua hatua kwa baadhi ya watu.

Amesema kuwa hata katika kipindi cha hivi karibuni Kuna watu wamekamatwa mkoani dodoma kwa makosa Kama hayo hivyo tunamshukuru waziri kwa maagizo yake na hatutalala kabisa.

Pia ameongeza kwa kuwataka wananchi kuendelea kujitokeza kwenye banda la BRELA ili kufanya sajili mbalimbali ili kujihakikishia na kile ambayo anakimiliki nanyi waandishi wa habari endeleni kuwahabarisha  wananchi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages