NMB Tandahimba Wazindua Huduma Tatu Mpya - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, October 5, 2020

NMB Tandahimba Wazindua Huduma Tatu Mpya

  DC Sebastian Waryuba akizindua wiki ya huduma kwa wateja Nmb tawi la Tandahimba

Meneja wa tawi la Nmb Tandahimba Julietha Ndazi akifafanua huduma mpya walizoanzisha kwa wateja wao.

Afisa Mikopo wa benki hiyo Godluck Mteri akielezea faida ya huduma ya Bima inayotolewa na Benki hiyo kwa kushirikiana na Makampuni husika.

Washiriki na watumishi wa benki hiyo wakati wa uzinduzi

Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba  amesema benki ya Nmb iendelee kutoa elimu wa huduma hizo mpya ili ziweze kuwasidia wakulima na wananchi kwa ujumla


Akizindua wiki ya huduma kwa wateja ambayo inafanyika kila mwaka amesema wateja wanahitaji kupata huduma bora hivyo iendelee kuboresha zaidi huduma hizo

Naye Meneja wa Nmb tawi la Tandahimba  Julietha Ndazi amesema wameanzisha huduma mpya tatu ambazo ni whatsapp namba ambayo itamsidia  mteja kupata ufafanuzi wa huduma za NMB

Amesema ingine ni QR Code  ambayo inatoa nafasi kwa wateja kutoa mapendekezo ya uboreshaji wa huduma za kibenki na huduma ya tatu ni huduma ya kurudisha  token ya Luku kwa wateja ambao wamenunua  umeme kupitia NMB mkononi

"Huduma ya kurudisha token ya luku ilikuwa na changamoto kwa wateja wetu lakini kwa sasa tatizo hilo tumelitatua kabisa kea kuanzisha huduma hiyo" amesema Ndazi.

Aidha naye Afisa Mikopo Godluck  Mteri  amesema  mbali na huduma hizo zipo huduma za Bima mbalimbali ambazo zinatolewa na benki hiyo hivyo wakulima na wananchi wachangamkie fursa hiyo ili kuzilinda mali  zao kwa kuzikatia bima

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages